WATU
watano wamefariki dunia mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti
likiwemo la familia ya mama na watoto wake wawili waliofariki kufuatia
ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao wakiwa wamelala.
Kwa
mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya mrakibu mwandamizi
Barakiel Masaki, tukio hilo lilitokea Agosti 16 mwaka huu majira ya saa
4:55 usiku.
Alisema
wanafamilia hao wakiwa wamelala nyumba yao ilianza kuwaka moto na
kwamba walipoteza maisha kutokana na kukosa hewa kufuatia moshi mzito
ulioenea ndani ya nyumba.
Amewataja
wanafamilia hao waliokufa ni mama mzazi Upendo Paul(24) na watoto wake
ambao ni Tecra Paul (4) na Aman Paul wote wakazi wa Ilemi darajani
jijini Mbeya.
Masaki
alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo mpaka sasa bado hakijajulikana na
miili ya maremu hao imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mkoani hapa.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kutokana na majanga ya moto yanayotokea mkoani hapa.
Wakati
huo huo mkazi wa majengo Mkwajuni wilayani Chunya Sprian
Majiyashamba(58) anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kuumua mke
wake kwa kumchoma kisu kutokana ugomvi wa kifamilia.
Kaimu
kamanda Masaki amesema marehemu alifahamika kwa jina la Secilia
Dotabarabara(64) ambaye alichomwa kisu na mume wake kwenye titi la
kushoto na kusababisha kifo chake papo hapo.
Masaki
amesema kuwatukio hilo lilitokea Agosti 16 mwaka 2012 majira ya saa
4:00 katika kijiji cha majengo wilayani chunya na kutaja chanzo cha
kifo hicho kuwa ni ugomvi wa kifamilia.
Katika
tukio lingine mwanamke mmoja mkazi wa kijiji cha nyakazobe wilayani
Mbarali amemuua mume wake kwa kumpiga na kitu kitu kizito kichwani
kutokana kutokana na na ugomvi wa kifamilia.
Akielezea
tukio hili Masaki amesema limetokea Agosti 16 mwaka huu majira ya saa
3:00 usiku kijijini hapo,na kwamba Christina Msiyunga(24) alimuua mume
wake Geoge Lova(26) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani na kusababisha
kifo chake papo hapo.
Amesema
mtuhumiwa wa tukio hilio amekamtwa na atafikishwa mahakamani baada ya
uchunguzi kukamilika,aidha aliwaomba wananchi kutatua migogoro kwa
amani ili kuepukana na vifo visivyo vya lazima.
Kwa hisani ya Joachim Nyambo