Friday, August 17, 2012

Tuko tayari kumlinda Ulimboka -Jeshi la polisi

Jeshi la polisi limetoa kauli hiyo kutokana na hofu hiyo na kuhisiwa kwa kufichwa kwa kiongozi huyo mara baada ya kurudi nchini kutokea Afrika ya Kusini

Dk Steven Ulimboka, kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania ni siku ya nne tokea arudi kutokea nchini

Jeshi la polisi limesema endapo Ulimboka ataomba ulinzi kutoka ndani ya Jeshi hilo basi litakuwa tayari kwa ajili ya usalama wa kumlinda

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela amesema, hawawezi kumpa ulinzi moja kwa moja bila yeye mwenyewe kuomba.

"Hatuwezi kumpa bila kuomba, na endapo atahitaji tutampa, sababu tunahofia huenda ukafanya hivyo halafu akasema hahitaji hilo, itakuwa ni fedheha kwa jeshi la polisi

Naye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleman Kova amesema wanashindwa kumpa ulinzi moja wka moja kwa kuwa tayari madaktari waliomba ulinzi kutoka UN.

Imedaiwa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kiliomba ulinzi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) jijini Dar es Salaam kwa kile kilichoadaiwa chama hicho hakina imani na jeshi la polisi.

Dk. Ulimboka alikwenda nchini Afrika Kusini Juni 30 mwaka huu kwa matibabu baada ya kutekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye msitu wa Pande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Juni 27, 2012 na kumsabishia maumivu makali na kujeruhiwa vibaya mwilini.

Augusti 12 mwaka huu, majira ya jioni Dkt.Ulimboka alirejea nchini na kuonekana mwenye afya nzuri na kupokelewa kifalme na mbwembwe na watu kwenye uwanja wa ndege wa jijini Dar es Salaam


Chanzo:Nifahamishe