
Siku
hiyo mnamo saa 7 usiku askari wanyamapori walisikia milio ya risasi
katika eneo la Nyungwe Kilomita 5 ndani ya Pori la Burigi. Askari
walifika katika eneo la tukio maana walikuwa wakifanya doria karibu na
eneo hilo na kukuta majangili ambao walikuwa wamemulika tochi zenye
mwanga mkali.
Majangili
walianza kurusha risasi walipobaini kuwa askari wamewakaribia. Askari
Wanyamapori walijibu mapigo na mapigano hayo yaliendelea kwa muda wa
takriban saa moja kabla ya majangili kukimbia.
Ilipofika
saa moja asubuhi, wakati walipokuwa wanakagua eneo la tukio, askari wa
Wanyamapori waligundua kuwepo kwa maiti akiwa na bunduki aina ya gobore
na baruti. Askari Wanyamapori walitoa taarifa katika kituo cha Polisi
Biharamulo ambapo Polisi waliuchukua mwili wa Marehemu na kuupeleka
katika hospitali ya Biharamulo ambako mwili umehifadhiwa hadi sasa.
Hadi
leo hakuna mtu aliyejitokeza kudai kupotelewa na ndugu. Hata hivyo
uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu huyo anayekadiriwa kuwa na
umri wa miaka 20 hadi 28 anaweza akawa ni raia wa nchi jirani.
Uchunguzi unaendelea.
George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NAUTALII
16th Agosti 2012