Kwa
kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote
wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume
ambayo ni www.katiba.go.tz
Kusoma
Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na upungufu wake
na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria kuhusiana na
mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
1. 1. MAMBO YA KUZINGATIA
Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:
Mtu
yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki
katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini
amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo
atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.
(b)Utaratibu wa Utoaji Maoni:
Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama zifuatazo:
(i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti (www.katiba.go.tz) barua pepe ya Tume, ( katibu@katiba.go.tz This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. ), nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769
(ii)Utoaji
wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani
ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681
DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
Endapo
Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa
ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama
Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya
maoni iliyoandaliwa na Tume.
(c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:
Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv)
endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake
(ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).
Tume
inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la
uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu
raia wa Tanzania pekee.
Kwa maelezo zaidi bofya: http://www.katiba.go.tz/index.php/maoni-nje-ya-nchi