Monday, August 20, 2012

Mkuu Wa Mkoa Wa Rukwa Aonana Na Balozi Wa Kenya Nchini, Atembelea Majeruhi Wa Ajali Ya Fuso



 

 
 Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima hapo kabla akimtambulisha balozi wa Kenya kwa viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Rukwa Ofsini kwake alipoenda kumsalimia kabla ya kuonana na Mkuu wa Mkoa huo.
 
Kutoka kulia ni Afisa Mkuu wa Jeshi la Usalama Barabarani Mkoani Rukwa, Katibu Tawala Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Samson Mashalla, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa (RPC) Jakob Maruanda na Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Francis Kilawe wakiwa kwenye meza ya mazungumzo na Balozi huyo wa Kenya.
 
 
  
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Balozi wa Kenya nchini Tanzania Balozi Mutinda Mutiso ofsini kwake leo alipotembelewa na balozi huyo ambaye yupo Mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kudumisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya pamoja na kuangalia fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Mikoa ya nyanda za juu kusini. Balozi huyo anategemea kwenda Mkoa jirani wa Katavi ambapo pamoja na shughuli nyingine ataembelea Hifadhi ya Taifa ya Katavi. Mkuu huyo wa Mkoa wa Rukwa amemuhakikishia balozi huyo uwepo wa fursa nyingi za uwekezaji Mkoani Rukwa ikiwemo Kilimo, Utalii, Uvuvi, Elimu na Biashara. Alimueleza kuwa kazi kubwa inayoendelea hivi sasa ni utengaji maeneo maalum ya uwekezaji.

 

 

Balozi wa Kenya nchini Tanzania Mutinda Mutiso akielezea lengo la ujio wake Mkoani Rukwa mbele ya Mkuu wa Mkoa huo na viongozi wengine wa Serikali ya Mkoa mapema leo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo. Aliiomba pia Serikali ya Tanzania kujenga urafiki na wageni ili kuimarisha mahusiano mazuri amabayo yamekwishajengeka kati ya nchi hizi mbili za Tanzania na Kenya. Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimsihi balozi huyo na nchi yake ya Kenya kusaidiana na Tanzania kudumisha amani iliyopo ili Afrika ya Mashariki pawe pahala salama pa kuishi na kufanya maendeleo ikiwemo uwekezaji ambao hauwezi kustawi pasipokuwa na amani
 
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Dkt. Emanuel Mtika akitoa maelezo ya majeruhi kwa Mkuu wa Mkoa huo alipotembelea kuwaona kufuatia ajali mbaya iliyotokea jana na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.
 
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akimpa pole mmoja wa majeruhi walionusurika kwenye ajali hiyo mbaya kati ya ajali zilizowahi kutokea Mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa Mkoa alisikitishwa na ajali hiyo iliyomfanya apige marufuku usafiri unaohusisha mizigo na abiria kwa wakati mmoja.
 
               Mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali hiyo akiwa na watoto wake wawili wadogo
 
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akitoa agizo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo Jakob Maruanda mbele ya waandishi wa habari na viongozi wengine wa Mkoa huo akiwemo Katibu Tawala Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima, agizo ambalo limepiga marufuku usafirishaji wa abiria katika magari ya mizigo. Alimueleza kuwa yeyote atakayekutwa akisafirisha abiria kwenye malori ya mizigo achukuliwe hatua kali za kisheria kudhibiti ajali za namna hiyo kutokea.