Monday, August 20, 2012

Makamu Wa Rais Aswali Swala Ya Idd Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam



 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa salamu za Sikukuu ya Eid kwa waumini wa dini ya Kiislam, baada ya kushiriki katika swala ya Sikukuu ya Eid Mubarak, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa kwanza kushoto) Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, (wa pili kushoto) wakijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika swala ya Sikukuu ya Eid Mubarak, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo asubuhi
 
 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana  na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka katika viwanja vya Mnazi Mmoja baada ya kumalizika kwa swala ya Sikukuu ya Eid Mubarak, leo asubuhi.
 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, baada ya kumalizika kwa swala ya Sikukuu ya Eid Mubarak, iliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo asubuhi

                               PICHA NA IKULU