Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiangalia mpunga
ukitoka katika mashine ya kuvunia mpunga (Combine Harvester) baada ya
kuzindua mashine hizo katika shamba la kilimo la serikali huko Bambi
Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein (wa sita kushoto), akiangalia mashine ya kuvunia mpunga (Combine Harvester) baada ya kufanya uzinduzi wa mashine hizo, zilizonunuliwa na serikali ya Mapinduzi zikiwa jumla 14 katika kuboresha hatua za mapinduzi ya kilimo, katika shamba la mbegu Bambi, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Agosti 06.12.
(Picha na Ramadhan Othman, Ikulu)