MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA)
VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VILIVYOPIGWA MARUFUKU
Mamlaka
ya Chakula na Dawa inapenda kuwafahamisha watengenezaji, waagizaji,
wauzaji na wananchi kwa ujumla kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 88 (a) cha
Sheria ya Chakula, Dawa na
vipodozi-2003, inakatazwa, kutengeneza, kuuza au kusambaza vipodozi
vyenye viambato (ingredients) vyenye sumu au athari kwa watumiaji.
Kwa
kuzingatia kifungu hiki, viambato vifuatavyo haviruhusiwi kutumika
katika vipodozi vyote vinavyotumika Tanzania kutokana na athari
zinazoweza kutokea kutokana na matumizi
yake:-
·
· Bithionol
·
· Hexachlorophene
·
· Mercury compounds
·
· Vinyl chloride
·
· Zirconium – containing complexes in aerosol products
·
· Halogenated salicylanilides (di-, tri- metabromsalan and tetrachlorosalicynilide)
·
· Chloroquinone and its derivatives
·
· Steroids in any proportions
·
· Chloroform
·
· Chlofluorocarbon propellants (fully halogenated chlorofluoroalkanes) in cosmetic aerosol products
·
· Methyelene chloride
Wananchi
kwa ujumla wanaaswa kuwa matumizi ya Vipodozi vya aina yoyote kati ya
vyote vilivyoorodheshwa hapa
chini yanaweza kumsababishia mtumiaji madhara au kumletea athari kubwa
kwa sababu vipodozi hivi vimeonekana kuwa na kiambato kimoja au zaidi ya
kimoja vyenye sumu vilizoorodheshwa hapo juu.
Mamlaka
inawataka watengenezaji, waagizaji, wauzaji na wasambazaji wote wa
vipodozi wahakikishe kwamba bidhaa
zao (vipodozi) hazina viambato vilivyotajwa hapo juu na vipodozi hivyo
visiwe kati ya hivyo vilivyotajwa hapa chini. Pia wahakikishe kwamba
vipodozi vilivyotajwa hapa chini haviingizwi wala kutengenezwa hapa
nchini.
Mamlaka inawataka wafanyabiashara wa vipodozi na wananchi kwa ujumla kuviwasilisha vipodozi vilivyo na viambato
venye sumu kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) au kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kwa ajili ya uteketezaji.
“Cream” na “lotions” zenye kiambato cha “Hydroquinone”
1.Mekako Cream
2.Rico Complexion Cream
3.Princess Cream
4.Butone Cream
5.Extra Clear Cream
6.Mic Cream
7.Viva Super Lemon Cream
8.Ultra Skin Tone Cream
9.Fade - Out Cream
10.Palmer`s Skin Success (pack) Cream
11.Fair & white Active Lightening Cream
12.Fair & White Whitening Cream
13.Fair & White Strong Bleaching Treatment Cream
14.Fair & white Body Clearing milk – tight Cream
15.Maxi – Tone fade Cream
16.Nadinola Fade Cream
17.Clear Essence Medicated fade Cream
18.Peau Claire Body Lotion
19.Reine Clair Rico Super Body Lotion
20.Immediat Claire Maxi – Beuty lotion
21.Tura Lotion
22.Ikb Medicated Cream
23.Crusader Skin Toning Cream
24.Tura Bright & Even Cream
25.Claire Cream
26.Miki Beauty Cream
27.Peau Claire Crème Eclaircissante
28.Sivoclair lightening Body Lotion
29.Extra Clair lightening Body Lotion
30.Precieux Treatment Beauty Lotion
31.Clear Essence Skin Beautifying Milk
32.Tura Skin Toning Cream
33.Madonna Medicated Beauty Cream
34.Mrembo Medicated Beauty Cream
35.Shirley Cream
36.Kiss – Medicated Beauty Cream
37.UNO21 Cream
38.Princess Patra Luxury Complexion Cream
39.Envi Skin Toner - Cream
40.Zarina Medicated Skin Lightener - Cream
41.Ambi Special Complexion - Cream
42.Lolane Cream
43.Glotone Complexion Cream
44.Nindola Cream
45.Tonight Night Beauty Cream
46.Fulani Cream Eclaircissante
47.Clere Lemon Cream
48.Clere Extra Cream
49.Binti Jambo Cream
50.Malaika Medicated Beauty Cream
51.Dear Heart with Hydroquinone Cream
52.Nish Medicated Cream
53.Island Beauty Skin Fade Cream
54.Malibu Medicated Cream
55.Care plus Fairness Cream
56.Topiclear Cream
57.Carekako Medicated Cream
58.Body Clear Cream
59.A3 Skin Lightening Cream
60.Ambi American Formula Cream
61.Dream Successful Cream
62.Symba crème Skin Lite ‘N’ Smooth Cream
63.Cleartone Skin Toning Cream
64.Ambi Extra Complexion Cream for men
65.Cleartone Extra Skin Toning Cream
66.O`Nyi Skin Crème
67.A3 Tripple action Cream Pearl Light
68.Elegance Skin Lightening Cream
69.Mr. Clere Cream
70.Clear Touch Cream
71.Crusader Ultra Brand Cream
72.Ultime Skin Lightening Cream
73.Rico Skin Tone Cream
74.Baraka Skin Lightening Cream
75.Fairlady Skin Lightening Cream
76.Immediat Claire Lightening Body Cream
77.Skin Lightening Lotions Containing Hydroquinone
78.Jaribu Skin Lightening Lotion
79.Amira Skin Lightening lotion
80.A3 Cleartouch Complexion Lotion
81.A3 Lemon Skin Lightening Lotion
82.Kiss Lotion
83.Princess Lotion
84.Clear Touch Lotion
85.Super Max – Tone Lotion
86No Mark Cream
Jeli zenye kiambato cha “Hydroquinone”
1.Body Clear
2.Topi Clear
3.Ultra Clear
Mafuta ya maji ya kujipaka yenye kiambato cha “Hydroquinone”
1. Peau Claire Lightening Body Oil
Sabuni zenye “Hydroquinone”
1.Body Clear Medicated Antiseptic Soap
2.Blackstar Soap
3.Cherie Claire Body Beauty Lightening & Treating Soap
4.Immediate Clair Lightening Beauty Soap
5.Lady Claire Soap
6.M.G.C Extra Clear Soap
7.Topi Clear Beauty Complexion Soap
8.Ultra Clear Soap
Sabuni zenye Mercury and its compounds
1.Movate Soap
2.Miki Soap
3.Jaribu Soap
4.Binti Jambo Soap
5.Amira Soap
6.Mekako Soap
7.Rico Soap
8.Tura Soap
9.Acura Soap
10.Fair Lady Soap
11.Elegance Soap
Krim zenye Mercury and its Compounds
1.Pimplex Medicated Cream
2.New Shirley Medicated Cream
Krim zenye misuguano (hormones in steroids)
1.Amira Cream
2.Jaribu Cream
3.Fair & Lovely Super Cream
4.Neu Clear Cream Plus (spot Remover)
5.Age renewal Cream
6.Visible Difference Cream (Neu Clear – Spots Remover)
7.Body Clear Cream
8.Sivo Clair Fade Cream
9.Skin Balance Lemon Cream
10.Peau Claire Cream
11.Skin Success Cream
12.M & C DynamiClair Cream
13.Skin Success Fade Cream
14.Fairly White Cream
15.Clear Essence Cream
16.Miss Caroline Cream
17.Lemonvate Cream
18.Movate Cream
19.Soft & Beautiful Cream
20.Mediven Cream
21.Body treat Cream (spot remover)
22.Dark & Lovely Cream
23.SivoClair Cream
24.Musk – Clear Cream
25.Fair & Beautiful Cream
26.Beautiful Beginning Cream
27.Diproson Cream
28.Dermovate Cream
29.Top Lemon Plus
30.Lemon Cream
31.Beta Lemon Cream
32.Tenovate
33.Unic Clear Super Cream
34.Topiflam Cream
35.First Class Lady Cream
Jeli zenye steroids
1. Fashion Fair Gel Plus
2. Hot Movate Gel
3. Hyprogel
4. Mova Gel Plus
5. Secret Gel Cream
6. Peau Claire Gel Plus
7. Hot Proson Gel
8. Skin Success Gel Plus
9. Skin Clear Gel Plus
10. Soft & Beautiful Gel
11. Skin Fade Gel Plus
12. Ultra – Gel Plus
13. Zarina Plus Top Gel
14. Action Dermovate Gel Plus
15. Prosone Gel
16. Skin Balance Gel Wrinkle Remover
17. TCB Gel plus
18. Demo – Gel Plus
19. Regge Lemon Gel
20. Ultimate Lady Gel
21. Topifram Gel Plus
22. Clair & Lovely Gel
Mamlaka
ya Chakula na Dawa imeanzishwa chini ya sheria ya Chakula, Dawa na
Vipodozi na. 1 ya mwaka 2003 ili
kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa chakula, dawa za mitishamba,
vifaa tiba na vipodozi. Udhibiti huu unafanyika kwa kusimamia uagizaji,
utengenezaji, usambazaji, uwekaji vielelezo (lebo), uuzaji na uhifadhi
wa bidhaa hizi na vitu vinavyotumika katika utengenezaji
wake.
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
S.L.P. 77150, DAR ES SALAAM
SIMU: 022 2450512 /2450751/2452108
FAKSI: 255 22 2450793
E-MAIL:
tfda@tfda.or.tz