Kufuatia Wizara ya Maji kukaa kimya bila kujibu barua toka Ofisi ya
Mbunge kwa zaidi ya mwaka mmoja, nimeamua kuchukua hatua za kibunge
kwa kuwasilisha kwa Katibu wa Bunge, taarifa na maelezo ya hoja
binafsi kutaka Bunge, katika mkutano unaotarajiwa kuanza tarehe 12
Juni 2012, lipitishe maazimio ya kuwezesha uwajibikaji wa Wizara
husika na mamlaka zake katika kushughulikia masuala ambayo nimeyaeleza
katika hoja husika.
Ikumbukwe kwamba, tarehe 20 Mei 2012 nilitoa mwito kwa Waziri Profesa
Jumanne Maghembe kuueleza umma hatua saba za haraka zaidi za Wizara ya
Maji kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka
katika Jimbo la Ubungo na Jiji la Dar es salaam mara baada ya Waziri
kurejea ofisini kutoka katika ziara hiyo ya vyanzo vya ruvu juu na
ruvu chini na kufanya mikutano na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
(DAWASA) pamoja na Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO).
Nilichukua hatua ya kutoa taarifa kwa umma baada ya Wizara kuwa na
utendaji mbovu wa kutojibu barua ambapo katika kipindi cha kati ya
mwaka 2011 mpaka 2012 nimeandika jumla ya barua nne kwa Wizara husika
kwa niaba ya wananchi kwa nyakati mbalimbali bila kupata majibu
yoyote.
Katika ya hatua hizo ambazo Waziri nilieleza anapaswa kuzisimamia
katika Wizara ya Maji ni; Mosi, kuchukuliwa kwa hatua dhidi ya kashfa
ya taifa ya kati ya mwaka 2003 mpaka 2010 ambapo Serikali ilitekeleza
Mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka
Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam
Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) uliotumia dola milioni
164.6 hata hivyo mpaka sasa katika maeneo mengi mtandao wake maarufu
kama mabomba ya wachina hautoi maji.
Pili; kuwasilisha bungeni Mpango Maalum wa kuboresha huduma za
Majisafi na uondoaji wa Maji Taka katika Jiji la Dar es salaam
uliopitishwa mwezi Machi 2011 kwa ajili ya kuidhinishwa, kutengewa
bajeti kamili ya utekelezaji wa haraka katika mwaka wa fedha 2012/2013
na kusimamiwa ipasavyo kwa msukumo wa kibunge badala ya ahadi za
ujumla za kwenye ziara.
Tatu; Waziri kueleza hatua zilizopangwa kuchukuliwa kufuatia ziara
yake kuhakikisha Mpango wa dharura wa kupunguza kero ya maji ulionza
kutekelezwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na DAWASA kuanzia Juni
2010 unaohusisha uchimbaji wa visima 24 uliopaswa kukamilika Oktoba
2011 unawekewa muda wa ukomo wa kukamilika ndani ya miezi mitatu
katika maeneo ambayo miradi haijakamilika mpaka hivi sasa.
Nne; Waziri kukubaliana na pendekezo nililotoa bungeni kwa nyakati
mbalimbali la Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi
wa thamani ukilinganisha na ufanisi (Value for Money) wa Mradi wa
ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar
es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply
and Sanitation Project-DWSSP) kwa kurejea ukaguzi wa kiufundi
(technical Audit) uliofanywa na kampuni ya Howard Humphreys.
Tano; Waziri kuhakikisha Wizara ya Maji inaisimamia EWURA ifanye
ukaguzi wa kiufanisi (performance audit) wa miradi ya visima vya maji
takribani 200 ambavyo vilichimbwa na serikali na kukabidhiwa kwa
DAWASCO, jumuiya za wananchi na taasisi mbalimbali lakini haitoi
huduma inavyostahili kwa kadiri ya malengo ya awali. Aidha, Wizara ya
Maji ihakikishe EWURA inaharakisha kutunga kanuni za udhibiti wa ubora
na bei ya huduma ya maji kwa upande wa sekta binafsi katika Jiji la
Dar es Salaam.
Sita; Waziri kuwezesha Kamati husika ya Bunge ijadili taarifa ya
ukaguzi wa ufanisi kuhusu usimamizi wa usambazaji wa maji katika
maeneo ya mijini (performance audit report on the management of water
distribution in urban areas) ya Januari 2012 iliyotolewa na CAG kabla
ya mkutano wa nane wa bunge ulipangwa kuanza tarehe 12 Juni 2012 ili
maoni na mapendekezo yazingatiwe wakati wa mchakato wa bajeti.
Saba; Wizara ya Maji kuhakikisha Serikali inawasilisha kwenye mkutano
wa tisa wa bunge muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali
za majisafi na majitaka (Water Supply and Sanitation Miscellaneous
Amendment Bill) ili kushughulikia upungufu uliojitokeza katika
utekelezaji wa sheria zilizopo na kuweka mfumo thabiti wa usimamizi wa
sekta ya maji nchini.
Imetolewa Dar es salaam tarehe 8 Juni 2012 na:
John Mnyika
Mbunge wa Jimbo la Ubungo