"Ndugu zangu ila tukumbuke kuwa kama tunadai maslahi bora basi tujuwe uzalishaji wa tija lazima uongezeke tufanye kazi kwa bidii, ubunifu na tija" Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Eng. Ernest Ndikilo akijibu risala ya wafanyakazi wa mkoa wa Mwanza kwenye sherehe za mei mosi 2012 zilizofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Sherehe hizo zilianza leo asubuhi kwa maandamano na maonyesho ya kusisimua.
Makampuni ya Ulinzi nayo yalinangwa katika hotuba ya mkuu wa mkoa kwani baadhi yao yameshafikishwa mahakamani kutokana na kutowalipa stahiki wafanyakazi wake huku kesi nyingi zikiwasilishwa ofisini kwake.
Mfanyakazi Bora toka SAHARA Communication ya jijini Mwanza, wamiliki wa Star TV, Radio Free Afrika, Kiss FM, na gazeti la Msanii Afrika, mpiga picha mr. Maliganya anayepunga mkono akiwa na wadau wenzie kwenye maandamano hayo...swali ni kwamba sherehe wapiiii....?
Bodi ya madawa nchini MSD nao kwenye maandamano hayo.
TANAPA hawoooo..
TANROAD ujumbe wao ulikuwa 'Usijenge wala kufanya biashara au shughuli yoyote ndani ya hifadhi ya barabara'
TTCL nao wamo...
Katibu wa kanda TPAWU ambaye pia ni mratibu wa mei mosi Mwanza Cecil Haule akimkabidhi risala mh. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Eng. Ernest Ndikilo ambapo kwenye hitimisho risala hiyo imeiomba Serikali sambamba na kupandisha kima cha chini cha mshahara pia imeimba Serikali kupunguza kodi ya mapato kwa Wafanyakazi hadi kufikia asilimia 9 na kwa bidhaa mbalimbali ambazo ni muhimu kwa mahitaji ya kila siku.
Katika risala yao wafanyakazi wa jiji la Mwanza wametamka wazi kuwa hawaoni jitihada za dhati zinazofanywa na Serikali katika kupata ufumbuzi na kutatua matatizo ya msingi yaliyowahi kuwasilishwa Serikalini ili kuondoa kero kwa wafanyakazi na jamii kwa ujumla.
Waajiri wengi nchini wamegeuza kazi nyingi kuwa za vibarua tu, hivyo wafanyakazi wengi hawana ajira ya kudumu.
Wafanyakazi wa majumbani nao walihusika kwenye sherehe hizi na wakawasilisha kero zao.
TAFAKARI: Mfanyakazi wa Tanzania anafanyakazi miaka 30 ndani ya utumishi bila kuwa na uwezo wa kununua hata godoro anakuja mgeni na kufanyakazi nchini, ndani ya mwaka mmoja anamiliki nyumba, gari na anamradi wake wa ziada...
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Mshahara duni, kodi kubwa na mfumuko wa bei ni pigo kwa wafanyakazi"
PICHA ZOTE NA kwa Hisani ya Gsengo.
PICHA ZOTE NA kwa Hisani ya Gsengo.