Wednesday, September 08, 2010

Mambo hayawi kama tunavyodhani

Malaika wawili watembeaji walisimama usiku mmoja katika nyumba ya familia ya kitajiri. Familia ile ilikuwa na jeuri kubwa. Walikataa kuwaruhusu wale malaika kulala kwenye chumba chao cha wageni. Badala yake wale malaika walipewa kasehemu kadogo uchochoroni kweenye baridi chini ya nyumba ile ya familia ya kitajiri.

Wakati wanajiandaa kutandika kwenye sakafu ngumu kujiandaa kulala, malaika Mkubwa aliona kuna tundu ukutani wa sehemu ile na akaliziba. Malaika mdogo akauliza, “ kwa nini umeliziba tundu hilo wakati familia hiyo ni ya watu jeuri?” Malaika mkubwa akajibu: “Mambo siku zote hayawi kama tunavyo dhania”

Usiku ya pili wale malaika walikwenda kupumzika kwenye nyumba ya mtu masikini sana. Mtu huyo ni mkulima mwenye huruma sana, pamoja na mkewekewe . Baada ya kushirikiana chakula kidogo walichonacho, wale masikini waliwakaribisha chumbani kwao wale malaika ili wapate kupumzika vizuri usiku ule.

Wakati Jua lilipochomoza asubuhi ya pili yake, wale malaika walimuona yule mkulima masikini na mkewe wakitokwa machozi. Wakawauliza kulikoni? Wakajibu, “Ng'ombe wetu mmoja tu tulienae ambae maziwa yake ndio kipato pekee tunachokitegemea tumemkuta amekufa shambani.”

Yule malaika mdogo akakasirika na kumwuliza malaika mkubwa, “inakuwaje umeacha jambo hili litokee? Yule jamaa wa kwanza tuliyelala kwake alikuwa na kila kitu, bado akatunyima malzi na kutulaza nje kwenye baridi kali. Hata hivyo ulimsaidia kuziba tundu kwenye nyumba yake. Huyu jamaa wa pili ni mwenye kitu kidogo lakini alikubali kushirikiana nasi kila kitu. Lakini umemuachia ng’ombe wake ambaye ni tumaini lake afe. Kwa nini lakini umefanya hivi?”

Malaika mkubwa akajibu, “mambo siku zote huwa hayawi kama tunavyodhania. Tulipokaa nyumbani kwa yule tajiri, niliona kupitia lile tundu dhahabu nyingi sana chini ya nyumba ile. Kwa kuwa jamaa ni mjivuni na mwenye kiburi sana asiyetaka kujitolea kwa ajili ya wenzake, niliamua kuliziba ili asiione dhahabu hiyo. Usiku uliopita tulipolala nyumbani kwa yule jamaa masikini, malaika wa mauti alikuja na kutaka kuichukua roho ya mke wa jamaa yule. Nikaamua kumtoa ng’ombe wake badala ya mke wake.”

Wakati mwingine haya ndio mambo haswa yanayotokea kinyume na vile tulivyotarajia.
you must be the changes you wish to see in the world.