Wednesday, March 25, 2015

Mchungaji Anaswa Gesti Laivu akiwa na Mke wa Mwanajeshi



Mchungaji Anaswa Gesti Laivu akiwa na Mke wa Mwanajeshi
Dunia inaelekea mwisho. Mchungaji mmoja wa Kanisa la Pentekoste, raia wa Kenya aitwaye Pasca Mugambi hivi karibuni alinaswa chumbani 'live' katika gesti moja iliyopo Manzese Tip Top akiwa na mke wa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambaye ni muunini wake.

Chanzo kilicho karibu na mke wa mjeshi huyo kilisema kuwa mchungaji huyo alikuwa akifanya shughuli zake za maombezi mjini Dodoma na kwamba askari huyo alimuita ili ampe huduma za kiroho mama yake mzazi aliye mgonjwa, baada ya kuwa amefahamishwa kwake na rafiki yake mmoja.
 
"Mchungaji huyo alikuwa akiishi sehemu nyingine hapa Dar lakini akienda kila siku nyumbani kwa mjeshi huyo kumfanyia maombi mama yake. Sasa akiwa pale akavutiwa na mke wa jamaa akaanza kumtongoza, ikiwa ni pamoja na kumtumia picha zake mbalimbali za utupu," kilisema chanzo hicho.
 
Inadaiwa kuwa kitendo cha kutongozwa na mchunga kondoo huyo hakikumpendeza mwanamke huyo, ambaye aliamua kulifikisha suala hilo kwa mumewe ili wajue cha kufanya.
 
Chanzo chetu kinadai kuwa mwanaume huyo mwenye cheo jeshini, alimwambia mkewe kuwa asingependa kumuadhibu mchungaji huyo kwa kutumia cheo chake.
 
"Huyu mchungaji nilimtoa Dodoma baada ya kupewa namba zake na rafiki yangu mmoja ili aje kumuombea mama yangu ambaye ni mgonjwa, lakini sasa namshangaa amepeleka maombi mengine kwa mke wangu, anamsumbua sana kuwa anampenda, nataka nimkomeshe ili iwe fundisho kwa wachungaji wengine wenye tabia kama yake," alisema  mjeshi huyo
 

Baada ya kukubaliana na mumewe juu ya kumkomesha mkware huyo, mke alikubali ombi la mchungaji huyo (huku moyoni akiwa na lake jambo), mchungaji naye bila hiyana akajaa na kumuomba mwanamke huyo wakutane katika gesti hiyo tayari kwa kuivunja amri ya sita ya Mungu iliyo katika kitabu kitakatifu cha Biblia.

Akiwa na uchu, mchungaji huyo alitangulia ndani ya gesti hiyo (jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kibiashara) na kupewa chumba namba 103 na kumtaarifu 'bibie' kuwa alikuwa tayari amefika.
   
Wakati mawasiliano hayo yakifanywa, mjeshi huyo alikuwa na mkewe 'chobingo' wakimsubiri mwenyekiti  wa  mtaa.
 
Katika kundi lililowajumuisha mwenyekiti  na mume, walifika chumbani hapo baada ya muda mfupi wa kusubiri na walipogonga, mlango ulifunguliwa na kuwakuta wawili hao wakiwa wamekaa kitandani na tayari wameshavua nguo zao za juu, mchungaji akiwa na bukta na fulana.
 
Alipoulizwa na mwenyekiti sababu za kuwepo na mke wa mtu anayefahamiana naye, yeye akiwa mtumishi wa Mungu, mchungaji huyo alijibu kuwa aliombwa na dada huyo kumfanyia maombi.

 
"Jamani naomba mnisamehe, shetani alinitangulia nilitaka kufanya maombi humu ndani," alisema kwa kigugumizi mchungaji huyo.
 
Katika hali ya ujasiri mkubwa, mjeshi huyo alimchukua mkewe na kumsamehe mchungaji huyo, lakini akamuonya kuachana na mchezo huo kwani anaweza kupoteza maisha yake.