Monday, July 04, 2016

RC MAKONDA ALITOLEA UFAFANUZI SWALA LA MIPAKA YA KAZI YA MEYA NA MKUU WA WILAYA



RC MAKONDA ALITOLEA UFAFANUZI SWALA LA MIPAKA YA KAZI YA MEYA NA MKUU WA WILAYA
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa mwingiliano wa kazi kati ya Mameya na wakuu Wilaya husababisha kushindwa kuelewana.

Makonda ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya tano za jijini Dar es salaam, amesema kuwa Mkuu wa Wilaya anaweza kuingia katika Baraza la Madiwani au Katibu Tawala wa Wilaya na wakati mwingine kuweza kuzungumza jambo katika baraza la madiwani.

Amesema kuwa meya licha kufanya kazi hiyo anatakiwa kuwa na kazi nyingine  ya kumuingizia kipato ambapo ni tofauti na Mkuu wa Wilaya ambaye anamuwakilisha Rais.