JAMHURI                YA MUUNGANO WA TANZANIA
        WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
        |  |  |  | 
| Simu:                         +255-22-2112035/40 |                                  S.L.P.  9223 | |
| Nukushi:                         +255-2122617/2120486 Barua                        pepe:ps@moha.go.tz |        Dar es                          Salaam | |
|  | 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi                kupitia Idara yake ya Uhamiaji imewahamisha jumla ya                Maofisa na askari wa Idara ya Uhamiaji hamsini na tisa                (59) kutoka Ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam na wilaya zake                walikokuwa wakifanya kazi na kupelekwa sehemu mbalimbali                nchini.
        Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya                Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema                uhamisho huo umefanyika ili kuongeza ufanisi wa utendaji                kazi katika Idara ya Uhamiaji. 
        Kwa mujibu wa Jenerali Rwegasira                zoezi hilo la kuwahamisha Maofisa wa Idara ya Uhamiaji                linaendelea kufanyika nchi nzima ikiwa ni hatua za                kuboresha utendaji kazi na hivyo kuongeza ufanisi zaidi wa                kiutendaji.
        Jenerali Rwegasira ameeleza kuwa                watumishi wote waliopewa uhamisho wanatakiwa kuripoti                kwenye vituo vyao vipya mara moja na kutoa angalizo kuwa                mtumishi yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa visingizio                mbalimbali atachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo                kuachishwa kazi.
        Imetolewa na Kitengo cha                Mawasiliano ya Serikali.
        5 Juni, 2016 
         
