Sunday, June 26, 2016

EFM REDIO YAWAZAWADIA SHILINGI MILIONI 3 WAKAAZI WA TEMEKE


EFM REDIO YAWAZAWADIA SHILINGI MILIONI 3 WAKAAZI WA TEMEKE
Kupitia mchezo wa sakasaka unaochezeshwa na kituo cha redio cha EFM leo tarehe 26/06/2016 imewafikia wakazi wa Temeke ambapo wakazi kumi wa wilaya hiyo waliweza kusaka vitu vilifichwa katika eneo la Temeke Mwisho na kila kitu kina thamani ya pesa. Mshindi wa kwanza amejishindia kiasi cha shilingi milioni 2 viwango vingine vya pesa vilivyotolewa kwa washindi ni kuanzia elfu hamsini,laki moja mpaka laki mbili.
 Mmoja wa washindi akishuhudia kiasi alichoshinda, Kutoka kushoto ni Meneja wa matukio na mawasiliano Neema godlays Mukurasi akiwa na Chogo mmoja wa watangazaji wa kituo cha EFM redio.
 Meneja wa matukio na mawasiliano Neema godlays Mukurasi akimkabidhi mshindi Flora Kafunga pesa taslimu kiasi cha shilling Laki moja.
 Mshindi wa kwanza Bi.Doris Joseph aliejipatia kiasi cha shilingi milioni mbili akiwa katika pozi la picha.
Baadhi ya watu wakishuhudia jinsi washindi wanavyopatikana katika eneo hilo