Na Woinde Shizza,Karatu
Wananchi wa kijiji cha Malekichanda kilichopo katika kata ya Mang'ola wilayani karatu mkoani Arusha wamelalamikia kitendo cha serekali kufungia ziwa Eyasi na kusema kuwa kitendo hicho kimewafanya vijana wengi kukosa kazi na kinaweza kusababisha wananchi wa eneo hilo kukumbwa na baa la njaa kutokana na kumaliza chakula chote ambacho walikuwa wamekihifadhii kwa ajili ya chakula cha akiba akiba.
Hayo waliyasema leo wakati Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alipofanya ziara yakutembela na kukagua baadhi ya miradi inayofanywa na chama pamoja na kuongea na wananchi wa kata hiyo.
Walisema kuwa wanasikitishwa sana na kitendo cha mkuu wa wawilaya kuwasimamisha shughuli zao za uvuvi kwani ndizo walizokuwa wakizitegemea katika kujipatia kipato pamoja na chakula katika kijiji hicho na kata kwa ujumla.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina Kristopher Nyato alisema kuwa tangu marchi 19 walizuiwakufanya shughuli zao za uvuvi katika eneo hilo na kupewa masaa 24 kuondoka katika eneo hilo kwakile kilichodaiwa kuwa eneo hilo limekubwa na ugonjwa wa kipindu pindu.
"unajua mimi ni mfanya biashara nimetokea mbali nasio mimi tu tupo wengi naninavijana wangu ambao nimekuja nao hapa kwa ajili ya shughuli hii ya uvuvi sasa tarehe hiyo 19 mwezi wa tatu mkuu wawilaya alikuja apa na askari nakutupa masaa 24 tuwe tumeondoka kuhoji nini ni wakatuambia ni pachafu mara waseme kuna kipindu pindu tukawaambia kama ni pachafu watuache wakagoma wakasema tumesema muondoke ndiposisi kwa kuwa tunaogopa nakamaunavyojua wananchi tulivyo waoga tukaondoka na tulivyoondoka walituambia baada ya siku chache wangefungua lakini adi sasa apajafunguliwa tunateseka sana ata vyakula vyetu vya akiba tumemaliza yaani apa ni tabu tu"alisema Nyato
Kwa upande wa mwananchi mwingine aliejitambulisha kwa jina la Wiliam Jonas alisema kuwa mara baada ya ziwa hilo kufungwa wamekuwa wanaishi maisha ya kuomba omba ,wao kama wananchi wanagawana chakula walichokuwa wamekiifadhi na kinakaribia kwisha na vijana wengi walikuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika ziwa hilo wamekuwa wazururaji.
Akiongea na wananchi hao Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka alisema kuwa yeye kama katibu amesikia malalamiko yao naatayafanyia kazi kwa kukutana na mkuu wawilaya nakuona ni jinsi gani ambavyo wataweza kutatua tatizo hilo.
Gazeti hili halikuishia hapo ilibidi kumtafuta mkuu wa wilaya ya karatu Omary Kwaanq ili kuzungumzia tuhuma hizi nakusema kuwa kweli wamelifunga ziwa hilo kutokana na ugonjwa wa kipindu pindu ambao umeikumba wilaya yake .
Alisema kuwa mpaka sasa wilaya yake ina wagonjwa 70 wa kipindu pindu na wamefanya utafiti ukaonyesha wagonjwa wengi wametokea maeneo ya ziwa hilo.
"tumefanya utafiti kiukweli kwa kushirikina na mtaalamu wamagonjwa wa milipuko nakubaini kuwa maji yale ya ziwa yana chembe chembe za wadudu wanao eneza ugonjwa wa kipindu pindu hivyo tukaamua ni borakufunga ziwa ilo ili wananchi wasiendelee kuzurika na ugonjwa huo.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuona maji yale ya ule mto yana vimelea vya ugonjwa wa kipindu pindu ndio maana wakaona ni bora wafunge ziwalile ili wananchi wasiendele kupata ugonjwa huo hatari.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hiii leo wakati alipofanya ziara katika kata hiyo iliopo ndani ya wilaya ya karatu mkoani Arusha
Diwani wakata ya mang'ola Lazaro Gege akiwa anampa maelezo kwa ufupi ya mradi wa matofali kaimu katibu mkuu wa vijana CCM taifa
Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa ccm Mkoa Arusha Sabaya Lengai akiwa anaongea na wananchi wa kata ya Mang'ola hii leo wakati wa ziara ya kaimu katibu mkuu wa vijana taifa |
baadhi ya wananchi wakiwa wanaendelea kufatilia mkutano huo