Wafanyakazi wa DAWASCO na Muhimbili wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo leo asubuhi.
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiendelea na shughuli za usafi katika Hospiyali hiyo Leo asubuhi.
Wafanyakazi wa DAWASCO wakikusanya takataka wakati shughuli za usafi zikiendelea katika hospitali hiyo leo Asubuhi.
Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) limefanya usafi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa lengo la kudumisha ushirikiano, lakini pia kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli la kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchini.
Usafi huo umeongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi , Mkurugenzi wa Uuguzi na Ukunga wa Muhimbili, Agnes Mtawa pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja.
Usafi huo umefanyika katika maeneo yote muhimu ya Hospitali ikiwemo utoaji wa maji taka .
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo, Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi amesema zoezi la kufanya usafi lazima halina budi kuwa endelevu ili kuhakikisha maeneo yote yanakua safi lakini pia epuka magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtawa amewashukuru DAWASCO kwa uamuzi wa kuja kufanya usafi MNH ambapo ametumia fursa hiyo pia kuwaomba wafanyakazi wa Shirika hilo kujitolea kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wagonjwa ambao wanahitaji damu.
Pamoja na mambo mengine DAWASCO wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa ambao wamelazwa Hospitalini hapo ambao wanapatiwa matibabu .
Neema Mwangomo, Afisa Uhusiano, MNH.