Sunday, April 03, 2016

MIAKA MIWILI YA EFM REDIO



MIAKA MIWILI YA EFM REDIO
Efm redio (93.7 FM) kituo bora cha utangazaji mwaka 2015 chatimiza miaka miwili sasa tangu kianze kuruka hewani tarehe 02/04/2014 hadi sasa 2016 ikiwa na watangazaji mahiri na wenye uzoefu, lengo ni kutoa burudani kutosha, matangazo, vipindi bora na habari bora.

Kituo hiki cha redio kilianza na vipindi vinne lakini hadi sasa kina vipindi vingi ambavyo ni Joto la asubuhi, Sports headquarters, Uhondo, Ladha 3600, Ubaoni, E-sports, Genge, Lala bye, Mezani, Funga mtaa, Ngoma Reggae, Afropower , kipindi chaGospel pamoja na bustani ya watoto. 

Hivyo kimewapatia vijana wengi ajira na kuwawezesha katika maisha yao kwa ujumla pamoja na kuinua vipaji vya vijana wengi.

Kituo hiki cha redio kimekua na mafanikio makubwa kwa muda mfupi, kilichokuja na staili ya kipekee ya kuukuza na kuupa kipaumbele muziki wa nyumbani pamoja na singeli,Mchiriku na mnanda ambao ulisahaulika na kuonekana wakihuni katika jamii.

EFM redio inalisongesha ipo tayari na inajipanga zaidi kuhakikisha wasikilizaji wake wanapata faida na mafanikio zaidi kupitia redio hiyo ikiwa ni pamoja na kusikika nchi nzima, na lengo ni kuifikia jamii nzima hususani wanyonge wasio na pakusemea.