JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
KUH: KUAHIRISHWA KWA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA
Natumia fursa hii kuwataarifu wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa kuwa, kikao cha Baraza kilichokuwa kifanyike kesho tarehe 13 Aprili, 2016 kimeahirishwa mpaka tarehe nyingine itakayopangwa.
Kuahirishwa kwa kikao hiki, ni kutokana na sababu muhimu zilizo nje ya uwezo wa waandaji.
Naomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza, kwani naelewa kuwa, wajumbe wengi mlikuwa mmeshapanga ratiba zenu tayari kwa kikao cha kesho huku mkiahirisha shughuli nyingine.
Tarehe nyingine ya kikao itakapopangwa, mtaarifiwa mapema iwezekanavyo.
Jaji Francis S.K. Mutungi
MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA.