Tuesday, April 19, 2016

OPERESHENI YA KUONDOA OMBAOMBA YAGONGA MWAMBA, POLISI WAJIPANGA NA MKAKATI MPYA.



OPERESHENI YA KUONDOA OMBAOMBA YAGONGA MWAMBA, POLISI WAJIPANGA NA MKAKATI MPYA.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP.Simon Sirro akionyesha silaha mbili  kwa waandishi wa habari walizokamata kwa jambazi Shaban Ramadhan baada kupewa taarifa na wananchi leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,CP.Simon Sirro akionyeshakwa waandishi wa habari mitambo ya kutengeneza pombe aina ya Gongo leo jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
OPERESHENI ya kuondoa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam limegonga mwamba kutokana na kukinzana na baadhi ya mamlaka katika kuwaondoa watu hao.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam leo , Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam (CP),Simon Sirro amesema kuwa operesheni ya kuondoa omba omba limeshindikana kutokana na baadhi ya mamlaka kushindwa kuhusishwa.

Amesema kuwa wanaendelea kujipanga kwa kuhusisha mamlaka zote ili kuweza kutekeleza operesheni hiyo kwa ufanisi.

Amesema kuwa kuna omba omba wengine wameweza kuondoka baada ya tangazo kutolewa hivyo waliobaki waondoke kutokana na operesheni itakayoanza hata angalia uso wa mtu.

Jeshi Polisi limeweza kukusanya zaidi ya sh. Milioni 911 zimekusanywa katika makosa mbalimbali ya magari  pamoja na pikipiki katika jiji la Dar es Salaam.

Kamanda Sirro amesema kuwa hawajisifii kukusanya fedha hizo nia yao ni kuona watu hawafanyi makosa ya usalama barabarani.

Wakati huo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata jambazi sugu, Shaban Ramadhan (35) ambaye alikuwa anamiliki bunduki mbili za kivita SMG na risasi nane.

Kamishina Sirro amesema kuwa walipata taarifa kutoka kwa watu juu ya mtu huyo kumiliki silaha ambapo alikutwa na silaha moja huko moja ikiwa kwa rafiki yake wa kike, Fatuma Salehe (20).
Aidha jeshi la polisi limeonya wananchi kununua gari katika sehemu zinazotambulika na zinalipa kodi kutokana na kuibuka uhalifu watu kuuza gari zisizo kuwa zao.