Zaidi ya shilingi milioni 967 zimetolewa kwa kaya masikini zipatazo elfu 07 Wilayani Mufindi, ikiwa ni kipindi cha miezi 08 tangu kuasisiwa kwa mpango wa miaka 03 wenye lengo la kuzinusuru kaya masikini, unaoratibiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF wilani humo.
Afisa habari na mawasiliano wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, Ndimmyake Mpokigwa Mwakapiso, amesema, kuanzi kipindi cha mwezi Oktoba mwaka jana hadi mwezi huu. kiasi cha shilingi milioni 967 laki tisa tisini na sita elfu, zimetolewa kama ruzuku kwa wanufaika elfu 07 miatisa 51 kutoka katika vijiji na mitaa 94.
Akibainisha baadhi ya mafanikio waliyoyapata wanufaika wa mpango huo, amesema kupitia ruzuku wanayoipata baadhi yao wameweza kuanzisha biashara na shughuli za kijasiliamali, kununua pembejeo za kilimo ambazo huzitumia katika mashamba yao, kununua chakula, kusomesha watoto, kununua bati kwa kila awamu wanayopokea fedha ili kujenga makazi ya kudumu huku kaya Zaidi ya elfu 03 zikijiunga na mifuko ya bima ya afya.
Aidha, pamoja na mafanikio yaliyofikiwa, baadhi ya changamoto zinazojitokeza miongoni mwa wanufaika ni pamoja na kuzitumia fedha hizo kwenye ulevi, baadhi ya akinamama kutokuwa wawazi kwa kaya zao mara baada ya kupokea fedha huku baadhi ya wanaume wakiwanyang'anya wake zao fedha wanazopokea kwa matumizi ya kaya na kwenda kuzitumia kwa matumizi mengine ya anasa Jambo ambalo ni kinyume na malengo.
Mpango huu wa Kiserikali ulianza rasmi mwaka 2015 chini ya uratibu wa mfuko wa maendeleo ya jamii nchini TASAF kwa kushirikiana na halmashauri ya wilaya ya Mufindi, ukiwa na shabaha ya kuzinusuru kaya masikini zaidi zlizokuwa zikiishi katika dibwi la umasikini wa kupindukia Wilayani humo.