Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela akipima BP kwa madereva wa masafa wakati wa uzinduzi wa kituo cha Wenda |
Mwakilishi wa Impala Jorge Rico Grillo akizungumza na wanahabari |
Mwakilishi wa makampuni ya usafirishaji Bw Arif Abri akieleza faida ya vituo hivyo kwa madereva |
mkuu wa mkoa wa Iringa Bi Masenza akijiandaa kukata utepe |
Uzinduzi wa kituo cha Ilula |
Add caption |
Mkuu wa mkoa wa Iringa akipima BP |
Na MatukuiodaimaBlog
MADEREVA wa malori nchini wametakiwa kutumia vituo vya upimaji virusi vya UKIMWI (VVU) kwa hiari kupima afya zao katika vituo vilivyojengwa kandokando ya barabara kuu ya kuanzia Jijijini Dar es Salaam hadi Tunduma mkoani Mbeya.
Ria hiyo imetolewa juzi na mwakilishi wa makampuni ya usafirishaji mizigo Bw Arif Abri kutoka kampuni ya FM Transporter wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Ilula wilaya ya Kilolo na Wenda kilichopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa ,kuwa matumizi sahihi ya vituo hivyo itakuwa ni ukombozi mkubwa kwa madereva na familia zao.
Kwani alisema kuwa hakuna udereva salama kama madereva hawatakuwa na tabia ya kujua hali za afya zao kupitia vituo hivyo ambavyo pia madereava hao watavitumia kupima na kutibiwa bure magonjwa mbali mbali.
Alisema madereva hao wakijua afya zao itawawezesha kufanya maamuzi ya busara yanayoweza kusaidia mikakati mbalimbali ya serikali ya kupunguza hasara na vifo vinavyotokana vya ajali zinazotokana na madereva hao kutokuwa na afya njema.
Hata hivyo alisema pamoja na vituo hivyo kuwalenga madereva bado wananchi wanaozunguka vituo hivyo wataweza kupata huduma hiyo bure na kuwa huduma katika vituo hivyo itatolewa kwa haraka zaidi.
Huku meneja wa kampuni ya Impala Terminals Tanzania ambayo ni sehemu ya wadau hao, Jorge Rico Grillo alisema kampuni yao kwa kushirikiana na mashirika ya Puma Energy Foundation na Trafigura walitoa fedha kwa shirika la kimataifa linalojishughulisha na afya la North Star Alliance na kujenga vituo hivyo.
Alisema pamoja na vituo hivyo viwili, wadau hao wamejenga vituo vingine vinne katika mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya vilivyozinduliwa kwa nyakati tofauti wiki iliyopita.
Alisema lengo lao ni kuona madereva wanaotumia barabara hiyo inayokwenda hadi nchi za Malawi na Zambia wanakuwa katika mazingira rafiki yatakayowawezesha kupata ushauri na huduma mbalimbali za afya wakiwa safarini.
Mwakilishi wa shirika la North Star Alliance, John Mwachama alisema kwa kupitia vituo hivyo madereva watapata elimu ya afya, madhara ya dawa za kulevya na pombe pamoja na huduma bure ya upimaji na matibabu wa magonjwa mbalimbali ikiwemo VVU, kisukari na mengineyo jambo litakalowawezesha kuchukua tahadhari kabla na wakati wakitumia barabara hiyo.
Meneja Uendeshaji wa Puma Energy Tanzania, Lameck Hiliyai alisema kujengwa kwa vituo hivyo kutasaidia makampuni ya usafirishaji kuwatumia madereva wanaojali afya zao.
Akizindua vituo hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema vituo hivyo vitakuwa vya manufaa sana kwa madereva na wananchi walio jirani navyo kwani vinaongeza upatikanaji wa huduma zinazotolewa pia katika vituo vingine binafsi na vya serikali.Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza akizindua vituo hivyo alipongeza wadau hao kwa kujitolea kujenga vituo hivyo na kutaka watendaji wa vituo hivyo kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa badala ya kuanza kuiba madawa.
Vituo hivyo ambavyo pia vitatoa huduma kwa wananchi wanaovizunguka, vimejengwa katika mji mdogo wa Ilula, wilayani Kilolo na kijiji cha Wenda, Iringa Vijijini kwa msaada wa wadau wa sekta ya usafirishaji nchini watakaogharamia uendeshaji wake hadi mwaka 2018.