Maabara ya kisasa ya Lancet iliyofunguliwa mjini Moshi jirani na YMCA kwa ajili ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya Saratani. Mtafiti wa Magonjwa,Dkt Hemed Kalebu akimuonesha Kaimu mganga mkuu wa mkoa ,Dkt Japhet Boniface ,maeneo mbalimbali alipotembelea maabara hiyo iliyofunguliwa mjini Moshi.
Dkt Kalebu akileza jambo kwa kaimu mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Dkt Josephat Boniface katika eneo ambalo hutumika kumpokea mgonjwa anayefika kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Dkt Kalebu akionesha sehemu ya vifaa mbalimbali katika maabara hiyo ambavyo vimekuwa vikitumika kwa ajili ya kufanya vipimo.
Baadhi ya vifaa mbalimbali vilivyoko katika maabara hiyo ya kisasa iliyofunguliwa mjini Moshi itakayotumika kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali ambayo baadhi ya wagonjwa wamekuwa wakivifuata nje ya nchi. Kaimu Mganga mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Dkt Josephat Boniface akiwa katika picha ya pamoja na Dkt Hemed Kalebu pamoja na watumishi wengine wa maabara hiyo .Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.