Sunday, April 03, 2016

LA KWETU CONCERT, TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI 2016 KUFANYIKA NCHINI TANZANIA



LA KWETU CONCERT, TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA INJILI 2016 KUFANYIKA NCHINI TANZANIA
Linatarajiwa Kufanyika Tamasha Kubwa la Muziki wa Injili hapa nchini. Tamasha hilo limepewa jina la "LA KWETU CONCERT" na litafanyika katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Geita, Kagera, Shinyanga, Mbeya, Arusha, Dar es salaam na mingineyo.

Tamasha hilo linaandaliwa kwa Ushirikiano na Waimbaji wa Muziki wa Injili, Watangazaji na Waandishi wa Habari chini ya Kampuni ya FAMARA INTERTAINMENT ya Jijini Mwanza, ambapo wadau mbalimbali wanakaribishwa ili kufanikisha tamasha hilo ambalo litakuwa la aina yake.