Sunday, April 03, 2016

KUWA NA DAN NYINGI SIO TIJA YA UMAHILI WA KUICHAMBUA SANAA YA KARATE



KUWA NA DAN NYINGI SIO TIJA YA UMAHILI WA KUICHAMBUA SANAA YA KARATE
Umathubuti wa fikra na ujuzi wa mbinu za matumizi ya sanaa ya Karate na nidhamu yake, haijali cheo cha Dan na jinsi unavyo jidhani kama ni bora zaidi ya wengine kimafunzo. Bali, unyenyekevu usio na dharau na nidhamu ya mafunzo ya Karate ndio ufunguo wa maendeleo kimbinu na umahili wa kuijua sanaa hii kubwa kama bahari. 

Karate ni mwenendo wa maisha, na haitumiwi kunufaisha ajenda za kibinafsi katika kuisaidia jamiii ya wanafunzi wenye moyo wa juu katika kujifunza sanaa hii.
Hivyo, hata kama unadai una Dan kadhaa, bila ya ujuzi na umahili unao endana na cheo katika utumuaji wa mbinu za hali ya juu na ufafanuzi wake unaoendana na "Form" au muonekano wa "stances" na ubora wa matumizi yake, ni bure kudai cheo cha ngazi ya juu kama hauna vigezo vya ufundi wake.

Kwa mfano Tanzania, inawana-Karate au Karatekas waliobobea kimafunzo na wamekuwa wakifanya Karate kwa zaidi ya miaka therasini na juu, lakini bado wana vyeo vya ngazi ya chini mno kwa kukosa msaada wa mafunzo ya ngazi za juu, hasa Dan za juu, kawaida zinatolewa Japan. Kuanzia Dan ya tano, ngumu kuipata tu bila kwenda Okinawa, Japan au Japan kiujumla kuzingatia kwa mba hizo ni nguzo kuu katika mtindo, lazima kujuwa mengi yanayohusiana na chimbuko la Karate kama utakuwa na Dan za ngazi ya juu zaidi.
Sensei Rumadha Fundi anazaidi ya uzoefu wa Karate wa zaidi ya miaka 38 sasa na anashikilia Dan 3 "Sandan" toka Jundokan So Honbu, Dan 2 "Nidan" toka Jundokan Kyokai, na Dan 6 "Roku Dan" toka Tanzania Karate - Do Federation. 

Hivyo, kwa njia moja au nyingine, hata kama haujabahatika kuwa na mwalimu wa ngazi ya juu kabisa, kuendelea na mafunzo kuzingatia maadilifu ya mtindo ndio njia pekee ya kukunufaisha bila kujali cheo na Dan unazozikusanya, kama huendani ni ujuzi wa matumizi yake. Mafunzo ni mwenendo, pia hayana mwisho. 

 Pia, yapo matumaini makubwa sana kwa Tanzania kuwa na tawi litalokuwa chini ya uongozi wa Sensei Rumadha na marafiki wake wa zamani walio wahi kufanya mafunzo ya Karate pamoja tokea miaka ya 1978 hadi 1980 katika "Hekalu la Kujilinda -Zanaki Dojo" akiwemo Ankal Muhidin Isaa Michuzi kama anavyo onekana katika Kata "Shisochin". 
Sensei Rumadha, ataiwakilisha Jundokan Tanzania katika mwaliko wa "Gasshuku" semina ya Karate nchi za ulaya, itayofanyika mjini Lisbon, Ureno mwezi Juni 10 hadi  Juni 12, 2016. Msafara huo utawajumuisha walimu wa kuu toka Okinawa, Japan, kama vile, mwenye kiti wa Okinawa Goju Ryu Jundokan So Honbu, Sensei Yoshihiro "Kancho" Miyazato, Tetsu Gima Sensei na Tsuneo Kinjo Sensei. Semina hii itajumuisha walimu wote wa Jundokan nchi za ulaya.