Baraza la Michezo Taifa(BMT) kwa kushirikiana na wadau wa ngumi za kulipwa wameunda kamati ya muda kwa ajili ya kuratibu na kusimamia maendeleo ya mchezo huo ndani na nje ya Nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Bw. Mohamed Kiganja amesema kuwa wameamua kuunda kamati ya muda ya mchezo huo itakayoongozwa na Katibu Mkuu Yassin Ustaadh kutoka TPBO na Makamu katibu Mkuu Chaulembo Palasa kutoka Chama cha Ngumi za kulipwa Tanzania(TPBC) kwa sababu hakukuwa na chombo kimoja kinachoratibu Ngumi za kulipwa nchini.
"Tuliamua kukutana na wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa mapema mwezi huu wakiwamo TPBO, TPBC,TPBC Limited , PST na KBF ili tuweze kupata chombo kimoja imara cha kuratibu mchezo wa ngumi za kulipwa nchini" alisema Bw. Kiganja.
Aidha Bw. Kiganja ameongeza kuwa viongozi waliochaguliwa wafanye kazi kwa bidii na sio kuongea sana ikiwemo kuwasilisha katiba ya kamati hiyo ndani ya siku 90 ili kuweza kuufikisha mbali mchezo huo na kuiletea sifa na heshima Tanzania katika mashindano ya kimataifa.
" Natoa wito kwa viongozi wa kamati hii wasifanye mzaha katika suala hili ikiwa kama mwanakamati hawezi kufanya kazi aseme mapema ili achaguliwe mwengine kwa manufaa ya Taifa" aliongeza Bw. Kiganja.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa kamati hiyo Bw. Yassin Ustaadh amesema kuwa wapo tayari kufanya kazi na kuufikisha mchezo huo mbali katika Nyanja za kimataifa na kuwataka mashabiki wakae mkao wa kula.
Mbali na hayo Bw. Ustaadh amewataka waandaaji wa mapambano hayo ambao hawana sifa na vigezo kukaa mbali na shughuli hiyo kwani hawahitaji ubabaishaji katika tasnia hiyo vinginevyo watatumbuliwa.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es salaam kuhusu viongozi waliochaguliwa wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa , kulia ni Katibu Mkuu wa kamati hiyo Bw. Yassin Ustaadh.
Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Muda ya Mchezo wa Ngumi za kulipwa Bw. Yassin Ustaadh akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani baada ya kukabidhiwa kamati hiyo leo jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Taifa(BMT) Bw. Mohamed Kiganja hayupo pichani alipotambulisha viongozi waliochaguliwa wa kamati ya muda ya mchezo wa Ngumi za kulipwa , kulia ni Katibu Mkuu wa kamati.