Sunday, April 03, 2016

Jumuiya ya Wide Zanzibar na soka la Wanawake


Jumuiya ya Wide Zanzibar na soka la Wanawake
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja mstaafu Juma Kassim Tindwa, akikagua timu za mpira wa miguu wanawake, New Generation Queens ya Kwahani na Jumbi Sisters, kabla ya mechi kati yao iliyofanyika katika uwanja wa mpira Kinyasini mkoani humo. New Generation ilishinda 1-0.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
KUTOKANA na mvua kubwa iliyonyesha katika Mkoa wa Kaskazini Unguja jana, mwamuzi alilazimika kulivunja pambano la kirafiki lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kuhamasisha soka la wanawake katika mkoa huo. Pichani wachezaji wa timu ya New Generation Queens waliokuwa wakipambana na Jumbi Sisters wakitoka uwanjani. Hadi mchezo huo ulipovunjwa timu hiyo ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0.
Baadhi ya wananchi wa Kinyasini wakifuatilia mechi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Meja mstaafu Juma Kassim Tindwa, akizungumza na wachezaji pamoja na wananchi wa Kinyasini baada ya kuvunjwa kwa pambano hilo kufuatia mvua iliyonyesha wakati wa mchezo huo.