Monday, April 18, 2016

DARAJA LA KIGAMBONI LAWA KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII WA NDANI


DARAJA LA KIGAMBONI LAWA KIVUTIO KIKUBWA KWA WATALII WA NDANI
 Ripota wa Globu ya Jamii Sultani Kipingo leo katembelea Daraja jipya la Kigamboni ambalo na kukuta limegeuka kivutio kikubwa cha watalii wa ndani, ambapo mamia ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali za jiji na hata mikoani wamejazana darajani hapo kwa mamia kujionea suluhisho la tatizo la usafiri kwa wanaokwenda na kutoka wilaya mpya ya Kigamboni, mkoa wa Dar es salaam. 
Daraja hili lenye urefu wa mita 680 na amblo limeanza kujengwa mwaka 2012 linamilikiwa na mfuko wa jamii wa NSSF kwa asilimia 60 na Serikali asilimia 40. 
Ujenzi wake umeenda sambamba na ujenzi wa barabara ya kilomita 5.7  na gharama yake ni  kiasi cha Dola za Marekani 143.5, ambapo serikali imetoa asilimia 40, huku NSSF ikitoa asilimia 60 ya fedha zote. Designer wake ni Arab Consulting Engineers na wajenzi ni China Railway Jiangchang Engineering (T) Ltd & China Major Bridge Engineering Company.
 Familia ikipita njia ya waendao kwa miguu katika daraja la Kigamboni leo
 Mamia ya watalii wa ndani wametembelea daraja hilo ambalo lilifunguliwa Jumamosi kuruhusu wananchi wajionee, kabla ya kuanza kazi baada ya kufunguliwa rasmi Jumanne hii
 Wananchi wakifurahia daraja la Kigamboni leo
Taswira ya daraja la Kigamboni kutoka angani.