Mtaalam wa Jiografia kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo ambayo wana uwezo nayo ili yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika chuo Kikuu Ardhi na vyuo vingine leo jijini Dar es salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa sekondari katika shule mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za masomo wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu ya Sekondari.