Na Woinde Shizza,Karatu.
                      WAZAZI wa vijiji vya                  Kata ya Barai iliyoko Wilayani Karatu Mkoani 
                          Arusha                          wameiomba Serikali ya awamu yaa tano kuchunguza                          sababu za watoto wao kufanya vibaya katika                          mitahani ya kuhitimu darasa la saba. 
                  Wazazi hao wametoa                  kilio hicho kufuatia ufauulu duni wa mara kwa mara kwa                  watoto wanaohitimu darasa la saba ambapo wanafunzi hao                  wamekuwa wanahitimu wakiwa hawajui kusoma wala kuandika                  na kushika nafasi za mwisho kitaifa katika mtihani wa                  darasa la saba jambo ambaalo wanaliona kama kuwapotezea                  muda watoto hao ambapo wazazi hao wakiwa wanawaitaji                  kuwachungisha mifugo. 
                          Aidha Kata hii ya                      Barai yenye shule 12 za msingi ambapo kati ya shule                      hizo shule sita zimefanya vibaya kitaifa na                      zimeshikilia nafasi za mwisho kabisa kitaifa ambapo                      alisema shule sita izo zipo katika nafasi za shule                      kumi zilizofanya vibaya kitaifa katika mtiani wa                      darasa la saba kwa mwaka jana. 
                Mwandishi wa habari                      hii alitembelea shule tatu za Kata hiyo kujua sababu                      zinazosababisha kutafaulu kabisa kwa wanafunzi                      ambapo taarifa zinaonyesha kuwa kuwa shuke hizo zina                      walimu sita pekee ikiwa na maana kila shule yenye                      madarasa saba ina walimu wawili 
                Wakizungumzia                      sababu za shule hizo kufanya vibaya mmoja wa mwalimu                      wa shule ya msingi Gidamilanda Paul Hando alisema                      kuwa ni pamoja na umbali mrefu ambao wanafunzi                      wanalazimika kutembea wakija mashuleni ambapo                      wanatembea zaidi ya kilimeta 24 kwenda shuleni                      ,pamoja na 
                wanafunzi kutumia                      muda mwingi kuchunga mifugo badala ya kujisomea                      pindi wanapotoka mashuleni. 
                Aidha alibainisha                      kuwa mbali na tatizo la umbali mrefu pia wanafunzi                      wamkuwa wakisumbuliwa na tatizo la njaa kwani shule                      hizo zimekuwa hasipikii wanafunzi mashuleni mchana                      kutokana na kutokuwa na bajeti hiyo.
                Kwa upande wake mmoja                wanafunzi hao ambao alijitambulisha kwa jina la Gilony                Gitonyi alisema kuwa wamekuwa wanashindwa kusoma kutokana                na njaa pamoja na kukosa mda wa kujisomea pindi wanaporudi                nyumbani kwani muda mwingi wamekuwa wakiutumia kwa ajili                kuchunga mifugo pindi wanaporudi majumbani.
                        Akizungumzia swala                      hilo mbunge wa jimbo la karatu Willy Qambalo alisema                      kuwa kwa upande wake anaona suluhisho la kutatua                      tatizo hilo ni pamoja na kujenga mabweni ilikuweza                      kuwasadia wanafunzi kupata elimu ili kila mwanafunzi                      asome apoapo shuleni ili kuweza kujipatia muda wa                      kujisomea. 
                "unajua kujengwa                      kwa haya mabweni pia itasiadia kuwapata wanafunzi                      kirahisi ambao muda wamekuwa wakiacha masomo na                      kwenda kuchunga mifugo jambo ambalo linapingwa                      vikali na wazazi wa vijiji hivyo na pia wanafunzi                      hao watapata muda mrefu wa kujisomea na swala wao                      kupata njaa litapungua kwani kutakuwa na chakula                      shuleni kwa ajili yao"alisema Qakambalo
                Aidha Tafiti                      zinaonyesha walimu ,wenye utovu wa nidhamu watoro na                      walevi katika maeneo ya mijini ndio hupelekwa katika                      shule hizzo zilizoko maeneo ya porini kama adhabu                      kwao.Swali la kujiuliza je mwalimu huyu atakuwa na                      nia ya kuwafundisha wanafunzi?Kupelekwa kwa mwalimu                      huyu kama adhabu badala ya eyey kuridhia Kujua                      kusomaa na kandika kwa wanafunzi hawa itakuwa ni                      ndoto.
               
