Wananchi na wateja mbalimbali wazidi kuifurahia huduma ya Ongea Deilee inayotolewa na Vodacom Tanzania ambayo ilizinduliwa mapema mwezi uliopita ambayo inazidi kuwapa unafuu na kuwarahisishia mawasiliano watumiaji wa simu za mkononi nchini ambapo wengi wameielezea kuwa inaendelea kufanya maisha yao kuwa murua.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya watumiaji wa mtandao huo ambao wamejiunga na huduma hii wameielezea kuwa inawawezesha kuendelea kuwasiliana na ndugu jamaa na marafiki kadri wapendavyo ikiwemo kuongea masuala ya biashara kwa urahisi zaidi
Yusuf Shemdoe Mkazi wa Tanga amesema kuwa mwanzoni alidhani ni mzaha aliposikia kuwa kuna uwezekano wa kuongea bure kila siku lakini alipojaribu kujiunga amekuwa akiwezeshwa kuongea na marafiki zake na wafanyabiashara wenzake mara kwa mara bila kuingia gharama yoyote hata akiwa na shilingi 60 tu kwenye simu anaongea kwa muda wa dakika 1.
"Mimi na marafiki zangu ninaofanya nao biashara hapa sokoni Tanga ambao tuko mtandao wa Vodacom tunaendelea kufaidika na Ongea Deilee maana tumekuwa tukipatiwa muda wa maongezi wa kutosha wa kutuwezesha kuwasiliana bila kikomo kila siku".Alisema Shemdoe.
Naye Juma Abdallah Mosha mkazi wa Dar es Salaam amesema kuwa yeye na marafki zake wanaifurahia huduma hii kwa kuwa imelenga kuleta unafuu kwa mtumiaji wa simu tofauti na promosheni nyingine zinazowaingizia hasara wateja.
"Ukijiunga na promosheni hii unapata muda wa kutosha wa maongezi ya kibiashara na kirafiki ikiwemo MB za intanet,fikiria ukiwa na shilingi 600 unawezeshwa kuongea bure kwa dakika 70 pia internet unapata zaidi,hii inadhihirisha kuwa Vodacom imedhamiria kuleta unafuu mkubwa wa gharama za mawasiliano nchini.
Kwa upande wake Somi Kimario mkazi wa Arusha amesema kuwa kuwa japo sasa hivi gharama za mawasiliano zimeshuka lakini huduma hii ya Ongea Deilee imefanya mawasiliano kuwa ya bure maana muda unaotolewa kuongea bure unatosha katika maoengezi ya kifamilia na ya biashara.
"Sasa hivi naona saa ya ukombozi katika sekta ya mawasiliano imefika kwa kuwa kila mtanzania mwenye kipato cha juu na mwenye kipato cha chini wote wanaweza kufanya mawasiliano ya kutumia simu kadri wapendavyo inatufanya tuiunge mkono serikali ya awamu ya tano kwa suala zima la kutenda kazi kwa bidii kwani kazi haziwezi kufanyika bila kuwa na mawasiliano bora na Ongea Deilee ndiyo suluhisho na fursa ya kuongea bure.
Aliwataka wanatanzania kuchangamkia fursa kama hizi ili ziwasaidie kuboresha maisha yao "Mimi kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia promosheni za Vodacom,mara zote zimekuwa na mwelekeo wa kufanya maisha ya watumiaji wa mtandao wao kuwa murua".Alisema.