TIMU ya Afya Sports Bara na Afya Sports Zanzibar zimetoka sare bao moja kwa moja katika mchezo uliofanyika jana katika Uwanja wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es salaam.
Timu ya Afya Sports Zanzibar ilikuwa ya kwanza kutikisa nyavu na bao la kwanza lilifungwa na Haji Abdalah kwenye dakika ya 22 kipindi cha kwanza.
Katika kipindi cha pili timu ya Afya Bara ilifurukuta na kurejesha bao lililofungwa na Mesa, hatua iliyopelekea timu hizo kutoka sare ya bao moja kwa moja.
Katika hatua nyingine, timu ya Netibili ya Afya Bara imeifunga mabao 30 -29 timu ya Netiboli ya Afya Zanzibar kwenye mchezo uliofanyia kwenye Uwanja wa Netiboli iliyopo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mchezo huo ni Tamasha la Pasaka ambalo hufanyika kila mwaka kati ya Watumishi wa Sekta ya Afya Zanzibar na Watumishi wa Sekta ya Afya Bara kwa lengo la kuendeleza undugu na ushirikiano.
Mchezaji wa timu ya Afya Bara, Drisa akimtoka mchezaji wa Afya Zanzibar, Hassan Abdallah "Kimti" katika mchezo wa tamasha la Sikukuu ya Pasaka. Katika mechi hiyo timu hizo zilitoshana nguvu sawa. Afya Zanzibar 1-1 Afya Bara. Mchezo huo ulifanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Wachezaji wa timu ya soka Afya Bara na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mchezo.
Wachezaji wa Netiboli ya Afya Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mchezo. Afya Bara imeifunga Afya Zanzibar mabao 30-29. Mchezo huo umefanyika jana kwenye viwanja vya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).