Tuesday, March 29, 2016

SUMATRA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA MABASI 105 NA 36 YAFIKISHWA MAHAKAMANI.


SUMATRA NA JESHI LA POLISI WAKAMATA MABASI 105 NA 36 YAFIKISHWA MAHAKAMANI.
Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
MAMLAKA ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi nchini wamekamata mabasi 105 yenye makosa mbalimbali na mabasi 36 yamefikishwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazo wakabiri.

Hayo yamesemwa na Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa Madereva na Makondakta wa mabasi hayo wamefikishwa katika mahakama za Kinondoni na Ilala jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kutokana na Operesheni inayofanywa na 
Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA) ikishirikiana na Jeshi la Polisi nchini imekuwa ikibaini baadhi ya madereva wanaokiuka Masharti ya leseni ya Kusafirisha abiria na wengine kutokuwa na leseni ndio maana wameona kuchukua hatua hiyo ya kukamata na kuwapeleka mahakamani madereva na Makondakta wanao kiuka masharti ya leseni zao.

Pia amewaasa wamiliki wa mabasi na wafanyakazi wakiwemo madereva na Makondakta wa mabasi ya Daladala kuzingatia masharti ya Leseni za usafirishaji wanapotoa huduma ya usafirishaji kwa umma na wananchi kwa ujumla wamewaomba kutoa ushirikiano pale ambapo wanaona madereva wanakiuka masharti ya reseni za usafirishaji, kuongeza nauli, kukatisha njia au kutumia njia ambayo haijapangwa na Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA).
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kukamatwa kwa mabasi yanayobainika kuvunja Masharti ya Reseni nyakati za asubuhi na jioni jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa mabasi 36 yameshakamatwa na kesi zao zipo mahakama ya Kinondoni na Ilala jijini Dar es Salaam.
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa nchikavu na Majini (SUMATRA), David Mziray akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kulia ni Afisa habari wa Idara ya Habari MAELEZO, Frenk Mvungi.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.