Sunday, March 20, 2016

RUVUMA TV @ TIZAMA MAGOLI YA MAJI MAJI NA MBEYA CITY YALIVOPATIKANA PALE MAJI MAJI WALIPOISHINDA MBEYA CITY 3 - 1




RUVUMA TV @ TIZAMA MAGOLI YA MAJI MAJI NA MBEYA CITY YALIVOPATIKANA PALE MAJI MAJI WALIPOISHINDA MBEYA CITY 3 - 1
Timua ya MAJIMAJI – WANALIZOMBE  imeendeleza ushindi kwa kuichapa  MBEYA CITY ya jijini MBEYA magoli matatu kwa moja. MAJIMAJI ndio waliokuwa wa kwanza kuliona lango la MBEYA CITY  dakika ya 14 kipindi cha kwanza DANNY MRUANDA akapacha goli wavuni. MBEYA CITY nao katika dakika ya 33 ya mchezo ikapata goli la kusawazisha kupitia

mchezaji wake ABDALA JUMA.Mpaka mapumziko MAJIMAJI moja na MBEYA CITY moja.
Kipindi cha pili katika dakika 64 ya mchezo, mchezaji wa MBEYA CITY akafanya makosa, ndipo MAJIMAJI ikapewa penati, walioyoitumia vema, na kupitia mchezaji  DANNY MRUANDA akaipatia timu yake goli la pili, dakika ya 78 ya mchezo MAJIMAJI ikapata goli la tatu kupitia mchezaji wake MASSELE BONIVENTURE. Mpaka mpira unamalizika MAJIMAJI WANALIZOMBE ikawa imefunga magoli matatu
na MBEYA CITY imefunga goli moja.

EBU TIZAMA MAGOLI YA MAJI MAJI MAJI NA MBEYA CITY YALIVOPATIKANA KUPITIA RUVUMA TV