Na Mwandishi Maalum, New York
Miaka 15 tangu kupitishwa kwa Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji kuhusu ubaguzi wa rangi na vitendo vingine vya aina hiyo. Kadhia ubaguzi wa rangi na asili ya mtu anakotoa bado inaendelea na kuongezeka
Mwishoni mwa Wiki hapa Umoja wa Mataifa palifanyika maadhimiyo ya siku ya Kimataifa ya kutokomeza vitendo vya kibaguzi: Changamoto na Mafanikio la Azimio la Durban.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alikuwa mmoja wa viongozi waliozungumza wakati wa adhimisho hilo, ambapo Mwenyekiti wa Kundi la Nchi za Afrika katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi alizungumza kwa niaba ya nchi za Afrika
Kwa ujumla viongozi wote waliozungumza walieleza kwamba pamekuwapo na mafaniko na changamato za utekelezaji wa Azimio la Durban na Mpango wa Utekelezaji miaka kumi na tano tangu kupitishwa kwake.
Baadhi ya mafanikio hayo kama ilivyoelezwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, ni pamoja na Nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa ama wametunga au kuboresha sharia zinazopinga vitendo vya ubaguzi, ukiwamo ubaguzi wa radi, Imani ya dini au asili ya mtu anakotoka.
Mafanikio mengine ameyataja kuwa ni yale ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana kutangaza Muongo wa Kimataifa wa Watu wenye asili ya Afrika ambao utaendelea hadi mwaka 2014 ikiwa ni sehemu ya kuenzi asili ya mtu mweusi, mila, tamaduni zake, ustawi na maendeleo yake.
Hata hivyo pamoja na juhudi zote hizo na safari ndefu ambayo jumuiya ya kimataifa imepitia tangu kupitishwa wa Azimio na Durban .Ban Ki Moon anasema vitendo vya ubaguzi ukiwao ubaguzi wa rangi, dini au asili ya mtu vinazidi kuongezea jambo ambalo anasema linampa wasi wasi.
" Naingiwa na wasiwasi sana namna wimbi la ubaguzi wa rangi, Imani ya mtu, au asili ya mtu linavyoongezeka. Kumekuwapo na ongezeko la maoni ya kibaguzi, vurugu na chuki duniano kote na vujo na vurungi dhidi ya kundi. Hii inaashiria kwamba bado hatujafanya vya kutosha na tuna safari ndefu.
Akabainisha pia kwamba mihemuko ya kisiasa na siasa za mrengo wa kulia navyo vinachangia kuondoa dhana ya kuvumiliana, lakini pia matatizo ya kiuchumi na ugumu wa maisha , wimbi la wakimbizi na changanoto wanazokumbana nao na kauli za kichochezi dhidi ya dini nyingine ni viashiria vingine vya dalili ya kuipeleka pabaya dunia.
Kwa upande wake Balozi Tuvako Manongi pamoja na kuungana na wazungumzaji wengine katika maadhimisho hayo kwamba Jumuiya ya Kimataifa imepiga hatua katika kujaribu kutokomeza ubaguzi na ubaguzi wa rangi bado watu wenye asili ya afrika wanaendelea kukabiliana na changamoto hiyo.
"Afrika inatambua ukoloni, ubaguzi wa rangi na dhuluma za kisiasa umesababisha ubaguzi wa kila aina na tabia ya kutovumiliana. Hadi leo hii Waafrika na Watu wenye asili ya Afrika na Watu wenye Asili bado wanaendelea kuwa waathirika dhuluma hii ya ubaguzi unao unakwenda sawia na ukosefu wa fursa za kiuchumi.u. Akasema Balozi Manongi.
Pamoja na changamaoto hizo kuendelea kuwapo miongoni mwa watu wa asili ya Afrika, amesema Kundi la nchi za African linashukuru kwa kupitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2015 Muongo wa Watu wenye asili ya Afrika: kwa lengo la kutambua haki, maendeleo , kukuza heshima, ulinzi na haki zote za binadamu na misingi ya uhuru wa watu asili ya Afrika.
Akaongeza Umoja wa Afrika unatambua na kuheshimu haki na uhuru wa kujieleza wa vyombo vya habari na mifumo mengine ya teknolojia ya mawasiliano yakiwamo mawasiliano ya internent na namna inavyoweza kusaidia juhudi za kukabiliana na vitendo vya ubaguzi wa rangi na vitendo vingine vya aina hiyo.
Hata hivyo akasema Afrika inahofu juu ya matumizi mabaya ya teknolojia mpya za mawasiliano, kama jukwaa la kuhubiri na kusambaza tabia ya kutokuvumiliana na vilevile kutumika kueneza namna mbalimbali za utumwa na biashara haramu ya usafirishaji binadamu.
Balozi Manongi, akaongeza kuwa Afrika inatoa wito kwa wamiliki na waendeshaji wa teknolojia ya mawasiliano kuweka sheria zitakazowabana watumiaji wanaokwenda kinyume na malengo mazuri ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi, akizungumza kwa niaba ya Nchi za kundi la Afrika katika Umoja wa Mataifa wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa kuhusu ubaguzi wa rangi miaka kumi na tano tangu kupitishwa kwa Azimio la Durban na Mapango wa Utekelezaji. Azimio hilo lilitokana na Mauaji yaliyotokea huko Sharpeville, Afrika ya Kusini mwaka 1960.
Mwakilishi wa Kudumu wa Antigua and Barbuda, Balozi Walton Alfonso Webson ambaye ni mlemavu wa kutoona,. akizungumza kwa niaba ya Kundi la Nchi za Latini ya Amerika na Visiwa vya Caribbian wakati wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya kutokomeza aina zote za kibaguzi ukiwamo ubaguzi wa rangi, dini au asili anayotoka mtu. Maadhimisho hayo yamefanyika mwisho mwa wiki.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akiwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bw. Mogens Lykketoft wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi