Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla leo 6 Machi amezindua rasmi utoaji wa viwanja kwa wanawake wa Mkoa wa Dar Es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambapo pia katika Mkoa wa Dar es Salaam maadhimisho hayo yakianza rasmi hiyo leo hadi hapo kilele 8 Machi katika viwanja vya Biafra.
Ambapo Dk. Kigwangalla ameelezea kuwa, maadhimisho hayo yanatoa fursa ya kuweza kufanya tathimini ya mafanikio ya kuwawezesha wanawake katika Nyanja mbalimbali na changamoto wanazokabiliana nazo.
Aidha, Dk. Kigwangalla katika tukio hilo,ametoa vyeti kadhaa vya umilikaji ardhi kwa wanawake vilivyotolewa na benki ya wanawake Tanzania (TWB. Pia amewaagiza maafisa maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha wanashinda kwenye jamii na kubaini kero na changamoto hasa wanazokumbana nazo wanawake na si kukaa maofisini ilikutoa hali na motisha kwa jamii ambayo asilimia kubwa imesahulika ikiwemo kufika ama kushiriki kwenye matukio kama hayo ya maadhimisho.
Dk. Kigwangalla hakufurahishwa na kitendo cha ushiriki mdogo wa wanawake katika shughuli hiyo huku maafisa wa maendeleo ya kijamii wakiwa ndio wenye jukumu lao na hawajachukua hatua yoyote ya kufanya hivyo katika kuwafikia wananachi na hata kuwaalika katika tukio kama hilo.
D. Kigwangalla ambeye alikuwa mgeni rasmi, pia aliweza kutembelea mabandambalimbali na kupata maelezo ya mabanda hayo ambayo asilimia kubwa yalikuwa ni ya wanawake mmoja mmoja na wale wa kwenye vikundi.