Thursday, March 17, 2016

AJALI YA BASI NA DALADALA JIJINI MBEYA LEO



AJALI YA BASI NA DALADALA JIJINI MBEYA LEO
Ajali iliyohusisha Basi la Kampuniya Ndenjela na basi ndogo aina ya Toyota Hiace, imetokea mapema leo asubuhi katika eneo la St Agrey Uyole, Jijini Mbeya na kupelekea watu kadhaa kujeruhiwa, huku wengine wakidhaniwa kupoteza maisha. Chanzo cha ajali hiyo, inaelezwa kwamba ni basi hilo dogo kuingia barabara kubwa bila ya tahadhali, hali iliyopelekea kugongwa na Basi hilo la Ndenjela lililokuwa safarini kuelekea Jijini Dar es salaam.Picha na Fadhil Atick MR PENDO, GLOBU YA JAMII, MBEYA