Ziko sababu kadhaa zinazoweza kuja muifanya serikali iiumbuke ikiwa ni pamoja na kushindwa kesi pale itaposhitakiwa.
Makosa ya serikali yenyewe
Kuna baadhi ya shughuli za serikali katika Taasisi na Mashirika ya Umma zimefanywa chini ya kiwango au kutotekelezwa kabisa kutokana na serikali kupeleka fedha kidogo tena kwa mafungu mafungu na wakati mwingine kutopelekwa kabisa licha ya kuwa Taasisi husika ilitengewa bajeti. Hili linaweza kuja kujitokeza katika Taasisi kama Bodi ya Mikopo na nyinginezo ingawa ursasimu,uzembe na utendaji mbovu wa watumishi unaweza kuwa sehemu ya tatizo
Influence ya wanasiasa
Kuna sehemu watendaji wanawajibishwa lakini mwisho wa siku uchunguzi unaweza kuja kubainisha kuwa kulegalega au utendaji mbovu katika Mashirika / Taasisi hizi kumechangiwa na maamuzi ya wanasiasa kuingilia utendaji wa ma-CEO,manegement na hata Bodi zinazosimamia Mashirika haya na hivyo itafika wakati baadhi ya ma-CEO hawa watakuja kuonekana hawana hatia na kulazimika kurudishwa kazini au kupangiwa kazi nyingine.
Sheria za Utumishi wa Umma
Kuna watendaji leo hii wanaweza kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi lakini taratibu na sheria za utumishi zikifuatwa,huenda baadhi yao ikaja kuonekana kuwa waliadhibiwa kimakosa na Mahakama ya kazi inaweza kuagiza warudishwe kazini mara moja.Serikali inabidi na ilipaswa kutazama vizuri sheria hizi za utumishi wa umma na kuzirekebisha kwanza kabla ya kuendelea na fukuzafukuza hii au huku kusimamisha watu kazi kila kukicha.
Agenda za Kisiasa
Wakati unakuja siasa hazitakwepeka katika hili zoezi la utumbuaji majipu. Wanaotumbuliwa waliwekwa na wanasiasa na wanaowatumbua ni wana siasa ila nao wana ya kwao hivyo itafika hatu mmoja akimwaga ugali mwingine atamwaga mbogo kwani sidhani kama kuna msafi miongoni mwao na wataanza kutoleana siri.
Wanaotumbuliwa kuamua kutoa ya mayoni:
Kuna baadhi ya wanaotumbuliwa ambao mambo yao yanaweza kuja kuisha kiani iwapo wataamua kufunguka kiasi cha kutaja majina makubwa na pale itakapoonekana mambo yameisha kiujanjaujanja, ndio serikali itajikuta ikiinyooshewa kidole na pengine hata kusutwa.Hawa wanaotumbuliwa wanaweza hata kupenyeza siri kwa waandishi wa habari.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu
Kushinda kesi nyingi zitakazoibuka hapo baadae kufuatia maamuzi yanayofanywa sasa na serikali,itategemea na ufanisi na uwezo wa Ofisi hii kusimamia kesi ambazo serikali inaweza kushitakiwa.Kama watakuwa hawajajipanga vizuri kwa kuwa na wanasheria competent na wa kutosha huku serikali ikikabiliwa na kesi nyingi,kuna hatari ya serikali kuja kushindwa kesi nyingi zitakazifunguliwa na watumishi,watu binafsi ama makampuni.Katika kipindi hiki, Ofisi hii inatakiwa ipewe kipaumbele kuliko Taasisi nyingine yote ya umma.
Ukifukuza watumishi,ukinyang'anya watu mashamba,ukivunjia watu nyumba na ukanyang'anya watu leseni,ofisi pekee itakayobeba mzigo wa kesi zitakazofunguliwa ni hii ofisi ya AG labda kama kuna utaratibu wa serikali kuweza kukodi makampuni binafsi ya uwakili kuisadia kusimamia baadhi ya kesi zitakazofunguliwa.
Maamuzi ya bila umakini
Hivi sasa mawaziri wako busy kusimamisha watu kazi na sidhani kama wanachukua tahadhari ya kutosha kabla ya kufikia maamuzi haya.Mfano mzuri ni kusimamishwa yule mtumishi aliyekuwa kiongozi wa bomoaboma alafa baada ya siku chache ikitako taarifa kuwa amerejeshwa katika nafasi yake(kama sikosei Nipashe ndio iliripoti habari ya mtumishi huyu kurudishwa kazini).
Kusimamia nidhamu na uwajibikaji ndani ya serikali ni jambo jema na linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo, lakini katika zama hizi za haki za binadamu na utwala wa sheria plus sheria zetu za utumishi wa umma, maamuzi haya ya leo yanaweza kuja kuwa "counterproductive " kwa serikali yenyewe yasipofanywa kwa umakini na kwa kutaka kujijenga kisiasa.
Katika kesi/mashauri kumi,serikali inatakiwa kushinda si chini ya saba au nane tofauti na hapo itakuja kuishi kubezwa kuwa ilikurupuka.
By Salary Slip/JF