Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akimjulia hali mmoja wa watoto waliolazwa kwenye wadi ya Watoto, Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza ili kujionea hali ilivyo Hospitalini hapo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akimsalimia mmoja wa mama aliyelazwa kwenye wodi ya kina mama wajawazito, Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando.
Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam akisikiliza malalamiko mbalimbali toka kwa wananchi waliofika Hospitalini hapo kupatiwa matibabu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu akizungumza na watumishi wa hospitali hiyo (hawapo pichani), ambapo amewasihi kutumia lugha nzuri wakati wanapotoa huduma kwa wananchi.
Baadhi ya watumishi wa hospitali ya mwananyamala wakimsikiliza waziri wakati wa majumuisho ya ziara hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh.Ummy Mwalimu, akiongea na wananchi wanaosubiri kuingia Hospitali ya Mwananyamala kuangalia ndugu zao.