Saturday, December 12, 2015

Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wawasili rasmi Wizarani baada ya kuapishwa


Waziri na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wawasili rasmi Wizarani baada ya kuapishwa
Waziri wa Mambo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Naibu Waziri wa Mambo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Suzani Kolimba akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha  Wizarani kwa mara ya kwanza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga mara alipowasili Wizarani baada ya kuapishwa Ikulu tarehe 12 Desemba, 2015. Aliyesimama pembeni ni Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo.
Mhe. Balozi Mahiga akikaribishwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya.
Mhe. Balozi Mahiga akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Nsia Paul wakati wa mapokezi yake Wizarani
Naibu Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Suzan Kolimba akipokea shada la maua kutoka kwa mmoja wa Watumishi wa Wizara Bi. Tagie Mwakawago mara baada ya kuwasili rasmi Wizarani
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimpokea Mhe. Waziri Wizarani. Pichani Mhe. Waziri akisalimiana na Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakimkaribisha kwa shangwe na furaha Mhe. Balozi Mahiga Wizarani.
Mhe. Waziri akisalimiana na Watumishi wa Wizara waliojitokeza kumpokea mara baada ya kuwasili Wizarani rasmi baada ya kuapishwa.
Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Mapunjo akijitambulisha rasmi kwa Waziri, Mhe. Balozi Mahiga na Mhe. Naibu Waziri, Mhe. Kolimba (kushoto).
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Simba Yahya akijitambulisha  rasmi kwa Waziri, Mhe. Balozi Mahiga na Mhe. Naibu Waziri, Mhe. Kolimba (kushoto). Mwingine katika picha ni Katibu Mkuu, Balozi Mulamula
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa akiongea jambo wakati wa mapokezi ya Mhe. Waziri na Naibu Waziri.
Waziri, Mhe. Balozi Mahiga kwa pamoja na Naibu Waziri, Mhe. Kolimba wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu, Balozi Mulamula na Bibi Mapunjo na Naibu Makatibu Wakuu, Balozi Yahya na Bw. Amantius Msole (wa kwanza kulia)
Picha ya pamoja
Picha na Reginald Philip