Saturday, December 19, 2015

WALIMU WASHIRIKI VYOO HIVI NA WANAFUNZI WAO KISA HIKI HAPA



WALIMU WASHIRIKI VYOO HIVI NA WANAFUNZI WAO KISA HIKI HAPA
vyoo
 

Jumla ya Wanafumzi 7I0 wa shule ya msingi Sunzula ( A) wilayani Itilima mkoani Simiyu walazamika kutumia tundu moja la choo na Walimu ambapo mahitaji ya choo ni matundu 28 hali ambayo imesababisha kukwama kwa ufundishaji na ujifunzaji na pia inaweza kusababisha milipuko ya magonjwa,hivyo jitihada zinahitajika kabla shule hiyo kufunguliwa januari mwakani .

Wakiongea na waandishi wa Habari walimu wa shule hiyo wamesema kuwa baada ya choo cha wanafunzi kuanguka, wanafunzi hao hawakuwa na njia mbadala ya kupata huduma hiyo na badala yake walilazimika kwenda porini kabla ya kupewa choo cha walimu.

Wamesema kuwa baada ya kugundua kushuka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni hapo na chanzo kikiwa ni ukosefu wa vyoo vya wanafunzi, walimu walilazimika kukigeuza choo cha chao chenye tundu moja kutumika kwa wanafunzi wa jinsia zote.

Kwa upande wake Mbunge wa Itilima Njalu Silanga ambaye yuko katika ziara jimboni mwake kujionea changamoto zilizopo aliyepita shuleni hapo amesema yeye atamalizia choo hicho kwa kujenga boma na kupaua lakini ameitaka jamii ya eneo hilo kuhakikisha inamalizia kwa kuyafunika matundu hayo vizuri ili yeye amalizie.