Na K-Vis Media/Khalfan Said.
MFUKO wa Pensheni wa PPF, umeibuka kidedea kwa kutwaa tuzo ya uwasilishaji bora wa hesabu zake katika kipindi cha mwaka 2014.
Katika hafla ya kutoa tuzo kwa taasisi za serikali na za watu binafsi, Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu, NBAA, imetoa tuzo hizo kwa makampuni na taasisi mbalimbali nchini, ambapo kwa upande wa kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, PPF ndiyo iliibuka ya kwanza ambapo Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko huo, Bw. Martin Mmari kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. William Erio, alipokea tuzo hiyo kutoka kwa mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Khamis Mwinyimvua. Pichani Bw. Mmari akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Khamisi Mwinyimvua.
(Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Martin Mmari, (katikati), akiwa amekamata tuzo wakati wa kupiga picha na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko huo kwenye hafla ya kutolewa tuzo ya taasisi iliyowasilisha taarifa za mahesabu za mwaka 2014 kwa kuzingatia taratibu na kanuni za mahesabu kwenye kituo cha mikutano cha Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa hesabu NBAA, huko Bunju nje kidoto ya jiji la Dar es Salaam, Desemba 5, 2015. PPF ilishika nafasi ya kwanza katika kundi la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Tuzo hizo hutolewa na NBAA.