Thursday, September 24, 2015

ZAIDI YA WATU 700 WAFARIKI KWA KUKANYAGANA, MAKKA-SAUDI ARABIA



ZAIDI YA WATU 700 WAFARIKI KWA KUKANYAGANA, MAKKA-SAUDI ARABIA

MAKKA (1)Waokoaji wakiwa katika harakati za kuokoa majeruhi wa tukio hilo.MAKKA (2)MAKKA (3)Shughuli za uokoaji zikiendelea.MAKKA (5)MAKKA (9)MAKKA (10)Umati wa waumini wa dini ya Kiislam waliokwenda kuhiji Makka, Saudi Arabia.MAKKA (11)Wakiwa wamefunika midomo yao kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kusambaa kwa njia ya hewa.MAKKA (13)MAKKA (14)MAKKA (15)MAKKA (18)MAKKA (19)

Waumini wa dini ya Kiislam wakiwa katika swala maalumya hija.

Makka, Saudi Arabia

ZAIDI ya watu 700 waliokuwa wakishiriki sherehe za Hijja wamefariki dunia na wengine zaidi ya 450 kujeruhiwa kwenye mkanyagano uliotokea katika mji mtakatifu wa Kiislamu wa Makka nchini Saudi Arabia.

Watu wengine wamejeruhiwa katika tukio hilo la kukanyagana lililotokea mji wa Mina, takriban kilomita tano kutoka mji wa Mecca. Mkanyagano huo umetokea siku ya kwanza ya kusherehekea sikukuu ya Eid al-Adha.

Idara ya ulinzi wa raia nchini humo imesema shughuli za uokoaji zinaendelea,  ambapo idara hiyo imejitahidi kukabiliana na tatizo hilo na kuongeza kuwa mpaka sasa imeongeza askari wa ulinzi na usalama wapatao 100,000 kwa ajili ya kuimarisha ulinzi.

Watu zaidi ya milioni mbili walisafiri hadi kwenye mlima Arafat jana asubuhi kwa ajili ya swala kama ishara ya Hijja.

Tukio hilo wa watu kupoteza maisha limekuja wiki chache baada ya winchi ya ujenzi kuanguka kwenye jengo la msikiti mkubwa zaidi duniani  jijini Makka na kuua watu zaidi ya 100 na wengine mamia kujeruhiwa.

NA DAILY MAILY