1. Mwezi Machi, 2015, Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Lilipitisha Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni Nchini Na.1 ya Mwaka 2015 (The Non - Citizens (Employment Regulation) Act). Sheria hii ilisainiwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei, 2015 na imetangazwa kuanza kutumika rasmi tangu tarehe 15/09/2015 kupitia Gazeti la Serikali Na. 406 la mwaka 2015.
2. Sheria hii inaanzisha Mamlaka moja ya utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni
na Mamlaka hiyo ni Kamishna wa Kazi.
3. Kwa kuzingatia matakwa ya Sheria hii, Wawekezaji au Waajiri wanaokusudia kuajiri wageni nchini wanapaswa kuwasilisha maombi kwa Kamishna wa Kazi na hati maalum ya kibali cha Ajira itatolewa kwa mgeni husika.
4. Mgeni atakayepatiwa kibali cha ajira atatakiwa kuwa na kibali cha Ukaazi ambacho kinatolewa na Idara ya Uhamiaji.
5. Ada ya Vibali vya Ajira italipwa kwa kuzingati aina ya daraja la kibali husika kama ifuatavyo;
i. Daraja A kwa Wawekezaji na waliojiajiri wenyewe-USD 1,000
ii. Daraja B kwa Taaluma maalum zilizoainishwa chini ya Sheria-USD 500
iii. Daraja C kwa Taaluma nyinginezo-USD 1,000
iv. Daraja D kwa walioajiriwa na Mashirika ya Dini na ya hisani-USD 500
v. Daraja E kwa ajili ya Wakimbizi- Bure.
Malipo au Ada ya huduma hii italipwa kupitia Akaunti inayotajwa hapa chini;
Name: Permanent Secretary, Ministry of Labour and Employment
A/C No: 0250211745400
Bank: CRDB
Aidha ,Mfumo huu mpya wa utoaji wa vibali vya Ajira kwa wageni utaanza rasmi tarehe 1/10/2015 na maombi yawasilishwe Ofisi ya Kamishna wa Kazi,makao Makuu ya Wizara ya Kazi na Ajira,jengo la NSSF-Mwl.Nyerere Tower,Na 42,iliyopo Barabara ya Bibi Titi Dar-es-salaam.
6. Wizara inapenda kutoa Rai kwa wadau wote kutoa ushirikiano ili kutekeleza matakwa ya Sheria kwa ufanisi wa maendeleo ya nchi yetu.
Imetolewa
Ridhiwani M. wema
Msemaji.
Wizara ya Kazi na Ajira.
28/09/2015