Kwenye mechi ya ufunguzi ya mabingwa wa EPL Chelsea dhidi ya Maccabi Tel Aviv, Jose Mourihno anategemewa kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kwa kuwaweka benchi mastaa wa timu hiyo.
Alithibitisha taarifa hizo Jose Mourihno alisema,"Ndio nitafanya mabadiliko kwasababu najaribu kutumia vitu tofauti. Ninatakiwa kuwapa nafasi wachezaji ambao hawachezi hivi sasa. Najua madhara yanayoweza kutokea kama ukiamua kufanya mabadiliko lakini naitaji kuwapa nafasi wachezaji wengine. Najua utasema kama nikimuacha Azpilicueta litakau tatizo, kama nikimuacha Terry itakua tatizo lakini hao wote wakiachwa nje ni matatizo yao wenyewe. Nina kikosi na nakiamini pia soko la wachezaji limefungwa na hatuwezi kubadilisha wachezaji ambao tumepoteza imani kwao. Ninakipenda kikosi changu lakini sina wachezaji 10 tu, sitakiwi kuwachezesha hao tu, ninatakiwa kufanya mabadiliko"
Mourihno pia alivyoulizwa kuhusu swala la yeye kuwa na wasiwasi alisema,"Mimi hivi sasa ni bingwa wa England, kwanini niwe na wasiwasi. Kuhusu UEFA ni mashindano mapya, kila mtu ana point zero na tunaanzia nyumbani hatutakiwi kuwa na wasiwasi"