Monday, September 14, 2015

IS YATEKA RAIA WA CHINA, NORWAY



IS YATEKA RAIA WA CHINA, NORWAY


Kundi la Dola la Kiislamu limesema hapo jana kuwa limewazuia mateka wawili raia wa China na Norway na limedai fidia ya kiwango kisichojulikana ili kuwaachia huru.



Kundi hilo limechapisha taarifa zote za mateka hao, pamoja na picha zao ambazo zimekuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii.

Waziri mkuu wa Norway, Erna Solberg amethibitisha kutekwa kwa raia wa nchi hiyo na kuongeza kuwa mtu huyo alitekwa nyara muda mfupi baada ya kuwasili nchini Syria mwezi Januari mwaka huu na kusisitiza kuwa Norway hailipi fidia.