Mchungaji Mtikila hajakidhi vigezo vya NEC hivyo jina lake limekatwa na hatoweza kugombea urais kupitia chama chake cha DP., Mchungaji Mtikila alifika ofisini hapo na bajaji baada ya muda mchache akaondoka haraka bila taarifa yoyote anapoenda, baadaye akarudi na kuingia ofisi za NEC. Lakini mgombea huyu amefika akiwa hana vigezo muhimu
1. Hana mgombea mwenza. 2. Hana dhamana ya milioni moja ambayo inapaswa kurejeshwa na fomu. 3. Amechelewa na amefika nje ya muda na vigezo vinginevyo vilivyohitajika hakuwa navyo.
Lubuva NEC: " Mchungaji Mtikila hujakidhi vigezo vingi vilivyotakiwa, hata dhamana ya fedha huna, una lolote la kuzungumza"
Mtikila:"Kwa Jaji nimeapa ila mgombea mwenza hajaapa, nimetimiza vigezo ila nimeshangaa nafika hapa naambiwa sijatimiza vigezo vingi"
Mtikila: "Mkurugenzi wa Uchaguzi Muongo nimekidhi vigezo, isipokuwa mgombea mwenza ambaye amepatwa na tatizo"
Mtikila: "Mgombea mwenza hajafika maana mke wake alipatwa na matatizo ya kuugua ndio maana hajafika."
Mtikila: " Kukosa kugombea sio kwamba nitakosa kwenda Mbinguni, hata mwaka 2010 nilionewa pia"
Baaday ya kushindikana hatimaye Mchungaji Mtikila alipanda bajaji na kuondoka ofisi za NEC