Tuesday, August 11, 2015

BREAKING NEWS: KITETO MABOMU NA RISASI KWENYE OFISI CCM ZA WILAYA YAVURUMA



BREAKING NEWS: KITETO MABOMU NA RISASI KWENYE OFISI CCM ZA WILAYA YAVURUMA

"Mabomu,risasi za moto zatumika ofisi za CCM Kiteto
• Gari la Ole Sendeka lavunjwa vioo,Ole Nangoro anusurika kichapo


• Nyumba yake yavamiwa na wanachama, wavunja taa na kumpiga mlinzi  

JESHI la polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara limetumia mabomu ya machozi na silaha za moto kuokoa aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro na Christopher Ole Sendeka pamoja na kamati ya siasa ya Mkoa wa Manyara waliofika kuhakiki matokeo ya Ubunge 
Awali wajumbe hao walizuiwa kwa mawe na magogo barabarani kata ya Engusero wasifike makao makuu ya wilaya ya Kiteto wakitokea Dodoma, hali iliyolazimu Jeshi la Polisi kuwaokoa kwa kuwapa ulinzi kwa kuwafikisha Kibaya kwaajili ya kuhakiki matokeo hayo
Baada ya kamati ya siasa ya mkoa kufika katika ofisi za CCM Wilaya ya Kiteto majira ya mchana walianza kuhakiki matokeo ya Ubunge ambayo yalidaiwa kulalamikiwa na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole Nangoro aliyeambatana na wajumbe hao kutaka yahakikiwe
"Baada ya kusikia kuna kamati ya siasa mkoa wa Manyara imefika wanachama tulilazimika kufika ofisi za CCM kutaka kujua hatma ya ujio wao, kwani tumeshuhudia maeneo mengi matokeo ya uchaguzi yanabadilishwa baada ya kutangazwa washindi"alisema mwananchi Rajabu Jagon"