Tuesday, August 11, 2015

BREAKING NEWS: Freeman Mbowe aongea na wanahabari baada ya kuugua ghafla jana akiwa kwenye maaandamano ya lowassa



BREAKING NEWS: Freeman Mbowe aongea na wanahabari baada ya kuugua ghafla jana akiwa kwenye maaandamano ya lowassa
mbowe
Freeman Mbowe akiongea na wanahabari leo. Kushoto ni James Mbatia.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mwenyekiti mwenza wa UKAWA Freeman Mbowe, ameongea na vyombo vya habari leo na kuelezea maendeleo yake kiafya baada ya jana kuugua ghafla na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Freeman Mbowe aliugua ghafla jana akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa baada ya kuchukua fomu za kugombea urais katika Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC).

Mbowe alishiriki katika maandamano yaliyoanzia Makao Makuu ya CUF yaliyopo Buguruni wilayani Ilala kuelekea NEC na baada ya Lowassa kuchukua fomu, mwenyekiti huyo aliendelea na msafara kwenda Kinondoni yalipo makao makuu ya Chadema.

Wakiwa njiani Mbowe na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walikuwa wamechomoza kwenye gari wakiwapungia wananchi waliojitokeza kwenye maandamano hayo.

Hali ya Mbowe ilibadilika ghafla na aliamua kushuka juu ya gari na kukaa katika kiti, ndipo Lissu na watu waliokuwamo kwenye gari hilo wakaanza kumpatia huduma ya kwanza kwa kumfungua vifungo vya shati lake katika eneo la Kinondoni kwa Manyanya na baadaye kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wakati hali ya Mbowe ilipoanza kubadilika msafara wa Lowassa ulikuwa ukielekea katika Uwanja wa Biafra, Kinondoni na magari yalikuwa yakitembea mwendo mdogo kutokana na maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana.


Source: JF