Monday, July 06, 2015

Zitto Kabwe Awataja Walioficha Mabilioni ya Fedha Uswisi


Zitto Kabwe Awataja Walioficha Mabilioni ya Fedha Uswisi

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo katika viwanja  vya Mwembeyanga jana amewataja watanzania walioficha mabilioni ya Fedha  katika Benki za nje ya nchi.
 
Akizungumza na  wakazi wa jiji la Dar es salaam Zitto Kabwe amesema  hivi sasa  uchumi wa nchi umeshikwa na watu wachache hususani wafanyabiashara ambao pia wameshika siasa au kwa wao kushiriki kwenye siasa moja kwa moja au kufadhili wanasiasa wa kutetea maslahi yao.
 
Ameongeza kuwa nchi ina Kansa ya Ufisadi ambapo  watu hutumia nafasi zao za uongozi kujilimbikizia mali ikiwemo  viongozi walioshika madaraka ya umma.
 
Mwezi Novemba mwaka 2012 Bunge lilipitisha Azimio namba Tisa la Mwaka 2012 ambalo lilielekeza Serikali kufanya uchunguzi kuhusu Watanzania na makampuni ya kitanzania waliotorosha na kuficha fedha kwenye mabenki ughaibuni
 
Uchunguzi pia ulikuwa uhusike na Mali za Watanzania zilizopo nje ya nchi katika juhudi za kuhakikisha kuwa fedha chafu na ufichwaji wake vinakomeshwa. Bunge lilitoa muda wa miezi sita kwa Serikali kufanya uchunguzi huo.
 
Mwaka mzima ulipita Serikali haikutoa maelezo yeyote na baada ya kubanwa ndani ya Bunge Serikali ikaomba miezi sita zaidi. Hata hivyo mpaka leo Serikali haijatoa kauli yeyote kuhusu taarifa hiyo ya uchunguzi.
 
Ametolea mfano kuwa  taarifa ya Serikali ya kisiwa cha Jersey kilicho chini ya himaya ya Uingereza inaonyesha kuwa Fedha na Mali za Watanzania katika mabenki kisiwani humo ni paundi za Uingereza 440 milioni ambazo kwa bei ya sasa ni sawa na shilingi za kitanzania 1.4 trilioni.
 
Vile vile taarifa rasmi ya Benki Kuu ya Uswiss inaonesha kuwa Watanzania wenye akaunti katika mabenki ya nchi hizo imefikia dola za kimarekani 304 milioni kutoka dola 213 milioni mwaka 2012. Amesema  hana takwimu kwa nchi nyingine duniani huku akisistiza kuwa fedha hizi  zilizofichwa zaweza kuwa halali au haramu.
 
Amesisitiza kuwa Serikali imenyima haki hiyo kwa zaidi ya miaka miwili na nusu sasa. Bunge la Kumi linavunjwa mnamo tarehe 9 Julai mwaka huu na hakuna dalili yeyote ya Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi ndani ya bunge kama ilivyoagizwa na Bunge.
 
Orodha hiyo amesema ali iwaslisha  kwa Gavana wa Benki Kuu, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya uchunguzi lakini Serikali mpaka sasa  haijatoa taarifa licha ya kupewa kila aina ya ushirikiano.
 
"Nimeamua leo kuiweka orodha hii wazi kama shinikizo kwa Serikali kutoa taarifa ya uchunguzi kabla ya Bunge kuvunjwa wiki ijayo."Amesema Zitto
 
Orodha hiyo ina majina 99 ya Watanzania au watu wenye mahusiano na Tanzania ambao wana akaunti HSBC ya Uswiss. Jumla ya akiba katika akaunti Benki hii pekee ni dola za kimarekani 114 milioni. 
 


Soma hapa kuona majina hayo……